November 7- Msanii mkongwe wa muda wote kutoka Afrika Mashariki, Mwanaisha Abdalla maarufu kama Nyota Ndogo anazidi kuiteka mioyo ya wengi kupitia ngoma zake. Nyota ambaye ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao wamepiga hatua kubwa kimuziki na kupata umaarufu kutoka nchi mbali mbali amedokezea kuendeleza burudani mwakani.

Akizungumza kupitia Kipindi chetu cha The Rush Hour siku ya Jumatano, Nyota amefunguka kwamba yuko na tamasha ambalo analiandaa kama njia moja ya kuleta wasanii pamoja na pia kusherehekea muziki wake kwani anaupenda sana.

Tamasha hilo ambalo amesema litafanyika mwaka ujao wa 2025 mwezi Februari siku ya wapendanao, amewahusisha wasanii mbali mbali.
Tamasha hilo litakalofanyika katika kaunti ya Taita taveta,litawajumuisha wasanii kama vile Kidis The Jembe, Dogo Richy, Chikuzee na Freshly Mwamburi.

Nyota amesema tayari ameongea na wasanii hawa na kukubaliana nao kwamba pesa atakayowalipa inatoka kwa Nyota Jikoni akisubiria kupata wafadhili zaidi kadri siku zinavyosonga.

“Nilianza kufanya hili tamasha mwaka uliopita na marehemu Ally B, mwaka huu sijafanya ila mwaka ujao nitakuwa nafanya na wasanii wenzangu. Si lazima tungojee shows za kuitwa,tunaweza tukaandaa matamasha yetu wenyewe,” amesema Nyota.

Nyota vile vile amesema kwamba kwa sasa hajaweka msanii wa kike ila ananedelea kumtafuta kwenye matamasha yajayo atawakumbuka pia japo anasema wengine wao huhitaji pesa nyingi ambazo Nyota Jikoni haina uwezo kwa sasa. Nyota amesisitiza kwamba pesa ambayo inamsaidia yeey kuendelea na shughuli zake za kila siku haitoki kwenye muziki bali kwa kazi yake ya kando.

“Mume wangu alisema hatanisapoti maana muziki haunilipi.Aliniambia kama ni biashara nyengine ya kando anaweza kunisapoti 100% kwa sababu anasema kama nanyimwa show,” ameongezea Nyota.

Amezidi kuwaomba mashabiki ambao wanamkubali kutoka kote ulimwenguni kumshika mkono kwa kununua tiketi ambazo ni shilingi 500 tu pekee na endapo mtu hataweza kuchukua tiketi, anaweza akatuma chochote hata hata kama ni mia moja.Amesema endapo watu watamshika mkono vizuri basi kiwango alichopanga kuwalipa wasanii wenzake kupitia Nyota Jikoni kitaongezeka na kuwapa motisha zaidi.

Nyota Ndogo hata hivyo amesema endapo kuna msanii angetaka kujitolea kuenda kutumbuiza bure hadi wakae waongee kwani haoni kama ni vyema msanii apande jukwaani kisha atoke bila ndururu.

Unaweza ukaanza kununua tiketi yako na mapema ama kumsapoti Nyota kupitia Paybill 400200 akaunti 852495.

Baadhi ya kazi ambazo Nyota Ndogo alipeta nazo kwenye soko la Muziki na pamoja na Watu na viatu ambayo ilimpatia tuzo mwaka wa 2007. Hadi sasa Nyota yuko na ngoma kwenye mitandao yake inayoitwa ‘Umetuangusha.’

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *