Nairobi, February 21- Mbwana Yusuf Kilungi maarufu Mbosso ambaye alikuwa kwenye lebo ya WCB afunguka baada ya kuondoka kwenye usimamizi huo wa Diamond Platinumz.
Mbosso ni miongoni mw wasanii ambao walikuwa wanafanya vyema kutoka hemaya ya Simba na amepata umaarufu mkubwa Afrika nzima.Kuondoka kwake WCB hakujakuwa na shida baada ya Diamond Platinumz kuweka wazi kwamba amemruhusu msanii huyo kuodnoka bila kumtoza hata ndururu tofauti na alivyoondoka Harmonize.
Kulingana na Diamond Platinumz,kumsamehe madeni msanii huyo ni kutokana na nidhamu na ushirikiano ambao wamekuwa nao kipindi wako pamoja.Simba amemsifia sana Mbosso na kumuombea heri njema na kusema kwamba bado wataendelea kushirikiana na kupeleka muziki wa Bongo Fleva juu zaidi.
Ikumbukwe kwamba miongoni mwa wasanii walioondoka Wasafi na baraka za Diamond ni pamoja na Rayvanny ambaye hata baada ya kuondoka bado wamefanya kazi kadhaa pamoja tofauti na Richi mavoko na Harmonize ambao tangu waondoke bado hawajafanya kazi pamoja na hawajawahi kuongeleana mema.
Mbosso hata hivyo ameweza kufunguka kuhusu malengo yake hata baada ya kutoka WCB kwamba sio kufungua lebo yake.Kupitia mahojiano na Ayo Tv nchini Tanzania,M<bosso amesema kwamba hana haraka ya kufungua lebo yake kwani hataki kuchukua msanii kisha ashindwe kumtoa kimuziki.
‘kuhusu kuanzisha lebo yangu sina haraka nayo,kwasasa najitafuta kwanza niwe imara kisha muda ukifika wa kmchukua msanii mwenzangu nitamchukua,sio vyema nichukue msanii kisha nishindwe kutimiza malengo yake.nawaona wengine walichukua wasanii lakini hawajawasaidia kwaiyo nisingetaka itokee,’amesema Khan.
Khan amefunguka pia kuhusu tatizo lake la ugonjwa wa moyo kwamba watu hawajui ila alizaliwa na ugonjwa huo.
‘Nimeishi na tatizo la moyo kwa takriban miaka 29,nilizaliwa nao,’amefichua msanii huyo.
Licha ya kuwa na tatizo hilo,mwamba amekuwa akijitahidi sana na wala hajawai acha show kisa kuumwa na moyo japo anasema alikuwa anapata maumivu makali sana baada ya kazi.Habari njema ni kwamba Mbosso ametangaza kwamba sasa hivi amepona tatioz hilo ambalo wataalam walisema ni ‘Umeme wa Moyo’ siku chache zilizopita akiwa katika hospitali ya Muhimbili.
Mbosso amefahamika kupitia ngoma zake kadhaa kama vile Tamba,picha yake,maajabu,tamu,hodari na nyenginezo.Amefanya kolabo na wasanii kutoka humu nchini kama vile Susumila kwenye ngoma yao ya Sonona.Mbosso ameachilia albums na ep kama vile Definition of Love ambayo aliachilia mwaka 2021 na Khan mwaka 2022 mtawalia.