Mombasa, Kenya, Januari 17- Msanii wa kike maarufu kutoka nchini Tanzania Zuhura Othman Soud maarufu Zuchu ambaye alizaliwa tarehe 22 Machi mwaka 1996 ni miongoni mwa wasanii waliojulikana kupitia lebo ya Wasafi Classic Baby(WCB) inayomilikiwa na Diamond Platinumz.

Zuchu anajulikana kwa sauti yake ya kipekee na umahiri wake katika muziki wa Bongo Flava, na amepata umaarufu mkubwa kupitia nyimbo zake kama “Wana” na “Sukari.”

Alianza kupata umaarufu baada ya kusaini mkataba na Wasafi Records, ambapo ameendelea kutamba katika muziki wa Afrika Mashariki na kimataifa. Msanii hyo wa kike ameweza kuzua gumzo kupitia mtandao wake wa Instagram baada ya kuandika ujumbe mrefu wa kutishia kuipeleka mahakamani Wasafi Fm inayomilikiwa na Diamond Platinumz.

Ameandika hivi; @diamondplatnumz KWAKO KIONGOZI Kinachoendelea sasa Mitandaoni kupitia maudhui ya kipindi chenu Mashamsham kimekua kama sehemu ya kuniumiza na kunididimiza kisanaa na kiafya ya Mwili Na akili. Lakini nasema nashukuru na nimeyapokea yote. Nimekua msanii wa taasisi mwenye kasi na mwenye kuipambania kazi yangu licha ya uwekezaji unaofanywa na kampuni yenu sikatai ni jambo kubwa na la kheri kumkomboa binti mwenye kipaji kwa kumuwekezea lakini nauliza Je ni haki hiko kutumika kama silaha pia.

Au niliwakosea nini mpaka kufikia kunifanyia Bullying na harassment hizi. Nasibu familia yako wanabaya langu lipi ambalo wanaona ni haki wao hata wakiwa na mahijiano binafsi kutokueka stara ya mambo yangu na huwa wanahakikisha hawakuharibii wewe bali mimi .

Nimefikia hatua leo Naandika barua ya kisheria Kwa walezi wangu sababu ya ukandamizaji wa mara kwa mara juu yangu Inauma sana .nitaenda mahakamani na pengine sitaweza kushinda taasisi yenu yenye nguvu lakini hata nikishindwa huko Namuachia MWENYEZIMUNGU yeye ndo Hakimu wa mwisho .

ASANTENI NASHUKURU kwa kuendelea kunibully na kuniharrass .Nishaomba Sana kwako kama kiongozi lakini mara nyingi maombo yangu hugonga mwamba na kunatengenezwa Contnt za kusudio la kunivunjia heshimq na Kuniumiza ,Na kuharibu afya yangu ya kiakili .mimi ni binti na Najua pia ni kwanamziki sijawqhi kuona media yoyote inaniharras kama ambavyo media ya taasisi yenu mmekua mkifanya . Sina cha kuwafanya kikubwa nyinyi ni wenye Nguvu Na mimi Namshitakia Mwenye Ukuu na utukufi zaidi Yangi na ninaenuamini zaidi M/MUNGU .ASANTENI SAN NASHUKURU  

Ameandika hayo kupitia Instagram yake kisha baadae kuufuta ujumbe huo. Chanzo cha ujumbe huo mrefu ni kupitia mahojiano ya kipindi cha MashamSham cha Wasafi fm ambapo kakake Diamond Platinumz alikuwa anafanyiwa mahojiano na kuzungumza kuhusu ndoa ya Zuchu na Diamond Platinumz jambo ambalo limemkwaza kidosho huyo.

Kufikia sasa,Zuhura amebadilisha maandishi kwenye bio yake ya Instagram yanamhusisha na usimamizi wa WCb Pamoja na kum-unfollow Boss wake diamond Platinumz.Asilimia kubwa ya mashabiki wanahisi hii itakuwa ni kiki tu huku wengine wakidhani zuchu ameihama lebo hiyo ya Simba.

Endapo zuchu ataihama Wasafi,atakuwa amefuata nyayo za Rich Mavoko,Harmonize na Rayvanny kuihama hemaya hiyo. Ikumbukwe kwamba wasanii wa bongofleva watakuwa na tamasha la serikali huko Dodoma nchini Tanzania ambapo kutakuwa na mkutano maalum wa chama cha CCm ambapo D.iamond Platinumz ni miongoni mwa wasanii watakaokuwepo

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *