Mombasa, Kenya, November 18- Mchungaji na pia msanii wa nyimbo za Injili amefunguka kuhusu muziki wake na safari yake kwa ujumla.Zablon K. Ndale ambaye alivuma mwanzoni mwa mwaka huu wa 2024 kupitia wimbo wake wa Mzabibu ameendelea kupata umaarufu humu nchini.


Akizungumza kwenye kipindi chetu cha The Rush Hour Ijumaa tarehe 15 Novemba, ameweza kufunguka kuhusu wimbo ambao ulimueka kwenye ramani wa Mzabibu.
“Mzabibu nilirekodi zaidi ya miaka kumi iliyopita kule Taita kwa studio ya Dickson Nyamawi ambaye pia alikuwa mtayarishaji wngu wa muziki. Yeye ndio amekuwa producer wangu kwasababu pia nilikuwa napenda kazi zake,” amesema Zablon.

Kulingana na Mchungaji ,hakuwa anatarajia kusambaa kwa ngoma yake ambayo imepeleka ujumbe kwa atu wengi tu ila hata pesa pia imeingia kupitia wimbo huo na mambo mengine kufunguka.
Baada ya mzabibu kuchezwa na watu mbali mbali ikiwemo viongozi na wanasiasa, Zablon anasema hakupata msaada wowote mkubwa japo anamshukuru mheshimiwa George Kithi kwa kumsimamia upande wa video.


“Walifanya challenge tu lakini hakuna zaidi ya hapo japo nawashkuru kwa hilo pia, siwezi kuwa na haya kumshukuru mheshimiwa George Kithi kwani amenishika mkono hata kunifanyia video ya wimbo huom,” Zablon Asema.


Mafanikio ya wimbo huo ni mengi na yameonekana kwani ngoma yake imekuwa ikichezwa na hata yeye kufanyiwa mahojiano na vituo mbali mbali vya habari nchini.Ameweza kupata nafasi hata ya kutumbuiza mbele ya Rais William Ruto mwezi uliopita kwenye sherehe za Mashujaa zilizofanyika kaunti ya Kwale.


Zablon anajivunia kwamba kwa sasa muziki wake unafikia watu wengi na ndio tamanio lake kwamba muziki ufikie wengi zaidi na kuwabadilisha na wazidi kuisambaza injili.

Kuhusu suala la kolabo na wasanii wengine hasa wa kizazi kipya,amesema kwamba aawajua vizuri wasanii ambao hata alikuwa nao siku ya Mashujaa akiwemo Dazlah,Kelechi,Mr bado na wengineo kwamba hakatai kufanya nao kazi lakini haiwezekani kwa sasa ikizingatiwa kwamba yeye anafanya muziki wa injili.


“Ili kufanya kazi na msanii mwengine hadi niangalie kama huo muziki utakuwa ni wa Injili.Nilikuwa na wasanii wengi tu lakini hatuna kazi yoyote na yeyote. Niko na nyimbo zangu zaidi ya 20 ambazo kwa sasa najaribu uwezo wa studio mpya baada ya ile ya Nyamawi kufungwa sasa mashabiki wakisema quality ya studio mpya iko sawa, naanza kurekodi,” amesema Ndale.


Amezungumza pia kuhusu wanakwaya wake wa Ajumbe a Bwana kwamba hajawasahau wala hatawasahau kwani alikuwa nao kule Kwale na kilem kidogo alichopewa aliwagawanyia pia.Kwasasa Mchungaji amesema ngoma atakazofanya lazima watakuwepo kwani ni watu wake ambao alianza nao.

Kwa sasa,Vindakala mbali mbali ndio jina la ngoma yake mpya ambayo imetoka mwezi huu na inaendelea kufanya vizuri.Kwenye wimbo huo,wanakwaya hawakuwepo studio ila ameweka sauti ya vijana wakishangilia kama njia moja ya kuhusisha pia vijana kwenye kazi zake za injili.


Ngoma hiyo inapatikana kwenye mitandao yote ya kuuzia muziki na ameahidi kwamba hata video yake pia haiko mbali kisha mashabiki wakikubali uzuri wa ngoma pamoja na studio mpya aliyorekodia,basi atakuwa anaendelea kudondosha kazi zake zengine.


Kwa sasa, Zablon anafanya muziki wa Injili kwa madhumuni ya kueneza injili bali sio kibishara tu.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *