Mombasa, Februari 6- Ramadhana Mnyaka Omar maarufu Winta rahalimz mzawa wa kaunti ya Taita Taveta ameendelea kuwa kwenye midomo ya mashabiki tangu aanze safari yake ya muziki miaka michache iliyopita.
Winta ni miongoni mwa wasanii wamaofanya vizuri na amekuwa kwenye mikono ya mtayarishaji muziki Emmy Dee.
Winta ni miongoni mwa wasanii wanaozungumziwa sasa hivi kupitia mitandao ya kijami baada ya picha na video kusambaa kwamba anapitia changamoto ya kiakili.Kulingana na video kwenye ukurasa wa facebook wa Tizo The Presenter, Winta ameeonekana akiwa mchafu kupitiliza katika maeneo ya Mwakirunge akiwa jalalani na magunia ya taka.
Kwenye picha,Winta anaonekana kutatizika kiakili huku wengine wakisema kwamba akili ‘imeruka.’
Baadahi ya wasanii kama vile Ashley Queen alikuwepo Mwakirunge kuona hali ya msanii ikoje hata hivyo baadhi ya washikadau wengine wa muziki wamehisi kwamba ni tukio tu la kuigiza.Miongoni mwa wasanii wanaohisi itakuwa ni maigizo tu ni Steve Kipande ambaye ameweza kuweka maoni yake kwamba sio kweli kwamba kijana yuko na changamoto ya akili.
Steve ameandika hivi; Huyu ni mzima mtu huchafuka after a very long time alafu seen the video kwa Tizo Waleoo the fake mwendazimu was looking down because he felt like laughing fakini.
Hivi unadhani Winta atakuwa anafanya kiki ama kweli anapitia changamoto?
Ikumbukwe kwamba,Wintaamekaa kwenye sanaa kwa takriban miaka mitano,amefanya kolabo kubwa na Kidis The Jembe kwenye ngoma yake ya ‘Tumekiwasha’ na anaendelea kufanya vyema.
Mwezi uliopita, msanii wa Hiphop kutoka hapa Mombasa ,Davy Gze alizua gumzo baada ya kuweka wazi kwamba yuko hospitalini kwa kuugua Malaria ambapo wasanii na baadhi ya mashabiki walihisi kwamba anadanganya na kuchukulia ni kiki.
Hivi utajuaje tofauti ya kiki nak isa cha ukweli?

Hali Ya Msanii Winta, Kweli Ama Kiki?
Shares: