Mombasa, Septemba 9-Nesphory Simbiga maarufu Kidis The Jembe ambaye amekuwa akizua gumzo mara kwa mara amekuja na jipya.Ngenje Kitaa ametangaza rasmi ujio wa tamasha lake ambalo atawaleta pamoja wasanii wote wanaokuja vizuri.
Kupitia mtandao wake wa Facebook,Kidis ameandika taarifa hiyo ambayo imepokelewa vyema na mashabiki huku wasanii wachanga wakihisi ni njia nzuri ya kufanya kazi na vipaji vyao pia viskike.
Kidis ameandika hivi:Guys Are You Ready For This?..All Coast Stars Artist Comes First Then The Rest Will Follow
… “The Jembe Festival” Coming Soon At Your Doors
..”Ngoma Draw & Bonge La Toto” As My National Anthem Oooooiiiii
..Wanga Wafe ..All 6 Counties With It’s Constituencies Get Ready #Mbulula Naja Na Kikosi Kizima Cha Wasanii Wa Sanaa Ya Kisasa
Kulingana na maandishi ya Ngenje Kitaa,tamasha lake halitakuwa la Mombasa pekee bali kaunti zote sita za pwani.Tamasha hili la The Jembe festival hata hivyo linatarajiwa kuvuka mipaka ya pwani kuwa la Kitaifa zaidi.
Macho yote sasa kwa Kidis akisubiriwa kutangaza msimamo rasmi kuhusu tamasha hilo.
Jukwaa ambalo anakuja nalo Kidis halina tofauti kubwa na Burudani Experience ya Kaa la Moto ambalo lilihusisha sana live performance ya wasanii mbali mbali kutoka ukanda wa pwani.Baadhi ya wasanii ambao walibahatika kutumbuiza jukwaa hilo ni pamoja na Echo254,Susumila,Kelechi Africana,Shirko,Manu Bayaz na wengineo.
Kufikia sasa,Kaa hajatoa tamko rasmi kuhusu kusitishwa kwa tamasha hilo licha ya kuanza kushika kasi.
Dj Lenium pia alianzisha tamasha la kila Alhamisi ambapo alikuwa anachukua wasanii wa zamani na wa sasa ila pia kidogo amekimya kwa sasa.
Ukizingatia mawazo ya baadhi ya washikadau,wote huitakia mema sanaa ya pwani japo changamoto za kifedha hufanya baadhi ya mambo kukwama.
Kule Tanzania,Wasafi Festival ni moja kati ya matamasha ambao hufanya vyema na kuekezewa pesa ndefu pamoja na kuungana kwa washikadau ili kuhakikisha kwamba inafanikiwa.
Je,washikadau watajitokeza kumuunga mkono Kidis?






