Mombasa, Kenya, December 10- Mitandao inazidi kuwaka moto huku kila mtu akitoa maoni yake kuhusiana na tamasha la Furaha City lililofanyika wikendi iliyopita Jijini Nairobi.
Kulingana a Willy Paul, wasanii wa humu nchini hawapewi heshima kama wanavyopewa wageni jambo ambalo liliweza kumskitisha sana. Ikumbukwe kwamba Tamasha hili lilipangiwa wasanii kibao tu wa kutumbuiza ikiwemo Khaligraph Jones, Mejja, Femi One, Ssaru, Trio Mio kutoka humu nchini huku Diamond Platinumz, Rayvanny na Zuchu wakiiwakilisha Tanzania.
Hatuna ripoti kamili ya ni nani alifaa kupanda jukwaani wa kwanza na nani alifaa kupanda wa mwisho ila kupitia video kwenye mitandao za Willy Paul, anasema kuna watu ambao ni wa humu nchini walikuwa wanamzuia na kumdhulumu kabla kupanda jukwaani.
Alivypanda kwa steji tu,alikataa kutumbuiza kupitia ngoma yake ya Mmmh aliyopmshirikisha Rayvanny na kumtaka Dj kuitoa na kucheza nyingine. “Wewe Dj toa hiyo takataka nipatie ngoma next,” alisema Willy paul akionekana kuwa na hasira. Kwa hali hii, Vanny Boy hakuonyesha chuki na bado alilopata nafasi alimuita Pozee japo hakutokea.
Tamasha hili limekuwa kwenye vinywa vya watu mashuhuri na wasanii mbali mbali kama vile Khaligraph Jones ambaye amemtaja Pozee kuwa jasiri na kusiamama na kauli yake.Mheshimiwa Peter Salasya akaandika kwamba ipo haja ya wasanii humu nchini kutoa ngoma nyingi zaidi kama Diamond Platinumz, director Trevor nae hajaachwa nyuma kwani aliandika kusikitishwa kwake na kutotumbuiza kwa Diamond Platinumz na kuitaja kama dharau.
Dj Shiti, Terence Creative, Akothee, Avril, Eric Omondi, Nadia Mukami, Bien ambaye alikuwa na tamasha nchini Tanzania ambalo alitumbuiza saa kumi na moja alfajiri pia ametoa maoni yake kwamba haoni sababu ya Pozee kuzua rabsha kwani angetumbuiza wakati aliofaa kutumbuiza.
Waziri Ali Hassan ni wa hivi punde zaidi kumtetea Willy Paul. Kupitia mahojiano na Obinna tv, Mheshimiwa Joho amesema kwamba yuko upande wa Willy Paul.
“Nasimama na Pozze kufa kupona,”amesema Joho.
Kule nchini Tanzania kumekuwa na vitisho kutoka kwa watu mbali mbali ikiwemo chawa wa Diamond Platinumz, Baba Levo ambaye pia ni mtamnganzaji wa Wasafi fm ambaye anasema kwamba Poze anatafuta kiki na Diamond platinumz hii ni baada ya meneja wa Simba kusema kwamba Pozze alikuwa anabishana na Zuchu wala sio Diamond japo anataka kuenda na upepo wa Simba.
Mwijaku ameweza kusema kwamba Pozze huenda asifanikiwe kimuziki na kuapa haswaa. Cassypool naye kutoka humu nchini amesema kwamba watu wasimdanganye Pozze.Bado watu wanachukua pande na kujitetea zaidi.
Hivi unadhani nani alifaa kupanda jukwaani wa kwanza? Na je kuna uzuri gani ubaya gani kupanda kwa steji wa mwisho?Je unapenda msanii wako apande wa kwanza ama wa mwisho ukienda kwa tamasha?