Mombasa, Kenya, January 14- Msanii na mwanzilishi wa kundi la Shemakimz, Shephard amekuwa kwenye maskio ya watu kwa zaidi ya mika kumi sasa.kundi la Shemakinz lilipeta kupitia ngoma zao zilizovuma kama vile Vijana Tunasota, Vumilia, Anisa, Kati Kati Yao na nyenginezo.
Mbali na kuwa msanii, shephard pia amejikita kwenye masuala ya biashara kama njia mbadala ya kuleta chakula kwa meza. Imefika mahali ambapo anafanya muziki kwa kuwa anaupenda ila zipo njia zinazompatia kipato.
Shephard pia hajaachwa nyuma kwani amefanya kazi akiwa pekeake na pia kushirikisha wasanii wengine ikiwemo Dazlah Kiduche na Teee Hits kwenye ngoma yake ya hiovi karibuni zaidi.Shephard alitangaza kuliamsha tena kundi lake mwaka huu kwani tayari kazi zipo kibao.
Msanii huyo mwenye asili ya Kaunti ya Kwale,ameweza kuzua gumzo kwenye mitandao baada ya kauli yake ya kumkataza mtoto wake wa kike kufanya muziki.Mishy beib ndio jina la kisanii la mtoto wake ambaye amekuwa akifanya vyema japo Shephard hataki.
Kupitia mahojiano ya njia ya simu kupitia kipindi cha The Rush Hour siku ya Jumatatu tarehe 13 Januari 2025, Shephard aliweza kueleza kwa kina sababu zinazofanya akatae mtoto wake kufanya muziki licha yay eye kuwa msanii.kulingana na Shephard,usanii una uchafu mwingi ambao si salama kwa mtoto wa kike huku akitaja kwamba kuna unyanyasaji na dhulma hasa kwa watoto wa kike.
“Sipendi mtoto wangu aendelee na usanii kwasababu watayarishaji muziki kama akina Tee hawawaachi salama. Angekuwa mwanaume nisingekuwa na shida lakini msichana apana acha ikae. Ujue nimekuwa kwa muziki kwa zaidi ya miaka 15 naelewa vile sanaa iko. Ataimbia nyumbani” ameongezea.
Hii imeleta mjadala mzito ikizingatiwa kwamba watu wanahisi kwa kuwa baba ni msanii, ingekuwa rahisi kumopatia nafasi na kumrithisha vikoba mtoto wake ili azidi kuskuma gurudumu ila hii imekuwa tofauti.Shephard ametilia mkazo suala la changamoto nyingi kwenye muziki ambazo hangetaka msichana wake azipitie.
Ikumbukwe kwamba wapo wasanii ambao wanawalea watoto wao kwenye njia za usanii walizopitia kama Daddy Q ambaye anamlea Marsh Mashav kwenye njia hizo.Fat S pia na mwanawe Hajj Mahela ni miongoni mwa wasanii wanaowalea watoto wao kisanii.
Wapo wengine am,bao wazazi wao si wasanii ila wamekumbatia sana ana kuwashika mkono wanao amba oni Pamoja na Shanarih Ecans ambaye anashikwa mkono na wazazi wake,Cebbuccah pia ameshikiliwa na wazazi wake,hivi unadhani kmipi kinafanya Shephard aghairi?