Mombasa, Februari 12- Nasha Travis, msanii wa kike kutoka humu nchini anaendelea kukua kwa kasi kutokana na muziki wake na kazi zake kwa ujumla na kuendelea kuwa kwenye midomo ya mashabiki kila kukicha.
Nasha ambaye yuko chini ya uongozi wa Ba’Nelson Empire, ni miongoni mwa wasanii wa kike kutoka kanda ya Pwani ambao wanaendelea kufanya vyema.
Kupitioa mahojiano kwenye kipindi cha The Rush hour, MoRadio, Nasha amefunguka kuhusu tetesi za kuwa kwenye mahusiano na Thee Pluto ambaye ni miongoni mwa Youtubers wakubwa na wafanyibiashara kutoka humu nchini.
Nasha ameweka wazi kwamba yeye na Thee Plito ni marafiki tu wala hawako kwenye mahusiano ya kimapenzi.
“Thee Pluto ni rafiki yang tu na tumejuana kwa muda wa miaka mitatu tangu nitoe ngoma na Mejja. Tumekuwa marafiki wazuri, tumekuwa tukisaidiana na kufanya kazi Pamoja,kufanya content,kupiga mapicha tangu kitambo akiwa na mpenzi wake Felicity,” amesema Nasha.
Kulingana na Nasha,watu wanamsingizia tu kwenye mitandao ila wawili hao hawajafikiria hata kuwa kwenye mahusiano.
Kwengineko, Nasha ameelezea jinsi gani ameweza kuwa kwenye muziki licha ya changomoto zilizopo kwenye sanaa,ameweza kuwashauri wasanii ambao wanaanza kuwa na watu wanaoweza kuwasaiodia kimuziki kama alivyo yeye.
“Kuna umuhimu wa kuwa na team ambayo inakusaidia kuskuma muziki wako na brand yako ndio maana mimi niko na team ambayo inanisaidia kama Nasha travis sio lazima ijue shida zangu personal kama Natasha,” ameongezea msanii huyo.
Nasha hata hivyo alifanya kazi kubwa sana mwaka jana ikiwemo kolabo na Okello Max lakini pia akavuka boda na kufanya ‘toto’ aliyomshirikisha Barnaba Classic.Ngoma hiyo ni miongoni mwa ngoma kubwa za mwaka 2024.
Haikuishia hapo, Nasha ameanza mwaka na ngoma mpya ‘Sisemi’ ambayo ameifanya na mtayarishaji muziki maarufu kutoka nchini Tanzania anayefahamika kama Mafeelings.Nasha anasema Sisemi ni miongoni mwa ngoma alizoandika kama miaka miwili iliyopita na zipo ngoma kibao ambazo ni mpangilio tu wa kuzidondosha.
Tutarajie Ep ama hata Album kutoka kwake mwaka huu.