Mombasa, Februari 26- Mtayarishaji maarufu wa muziki nchini, J Crack, ambaye amejiimarisha katika tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 20, ameachilia EP yake ya kwanza, Kilifonian Love, ambayo imevuma kwa kasi hasa kupitia mtandao wa tiktok.
Katika mahojiano ya kipekee na mwanahabari wetu, Yugebwize, J Crack alizungumzia kuhusu mafanikio yake na jinsi EP hii ilivyokuwa ya kipekee.
“Kilifonian Love ni EP bora zaidi, inajumuisha kila aina ya ngoma ambayo shabiki angetaka kusikiliza,” alisema J Crack, akisisitiza kuwa EP hii ni zawadi kutoka kwa wasanii kama Mr. Bado na Susumila kwa jitihada zake kubwa. “Waliona nimekuwa mwema kwao kwa muda mrefu, na walijua kuwa ni wakati wa kunishukuru,” alieleza.
Mfalme J amesema kwamba hiyo ndio EP yake ya kwanza tangu kuingia kwenye tasnia ya muziki nab ado yuko na ngoma zaidi ya 30 ambazo zipo tayari kuashiria kwamba watu waendelee kusubiri Ep yake ya pili hivi karibuni.
Kwenye mapato ya kazi hii amesema wasanii wake wote kila mmoja atapata kiwango flani kupitia Ep hiyo kwani wasanii wote kwenye Ep hiyo walijitolea na kumheshimisha tu kwenye kazi hizo.
‘Ep yangu kila msanii atapata percentage yake kwasababu wasanii wote kama vile Adasa nilimpigia simu na akasema hakuna haja tuongee sana wala kulipishana,Echo254 pia akanibless Pamoja na usimamizi wake huwa tunaongea sana,kwaiyo hii ni kazi ambayo imebeba upendo sana kuanzia wasanii hadi amshabiki,amesema Mfalme.
Pia, alifunguka kuhusu msanii mmoja ambaye alikuwa na mpango wa kumzindua rasmi, lakini alikutana na changamoto za kiakili ambazo zilimkwamisha. “Alikuwa na tatizo la kiakili, lakini sasa yuko sawa, na huenda EP ya pili ikawa yake,” alisema J Crack, akionyesha matumaini kwa msanii huyo ambaye anatarajiwa kuonyesha uwezo wake wa kipekee.
Pi a vile vile,amezungumza kuhusu changamoto ambazo wasichana hupitia kwenye sanaa ikiwa ni Pamoja na kukosa watu wa kumsimamia kazi zake.Ametaja baadhi ya watoto wakike ambao wapo kwenye muziki na watu ambao wanawasaidia kutimiza ndoto zao.
J Crack alizungumzia pia wasanii wanawake kama Nyota Ndoto, Adasa, Nasha Travis, na wengine, akisema kuwa wanafanya vizuri katika muziki kwa kuwa wana timu inayowasaidia. “Wana talent kubwa, lakini bila msaada wa timu bora, ni vigumu kufika mbali,” alisema.
J Crack alitaja pia kaka yake, Lai, ambaye kwa sasa ni mchungaji, kuwa mtu muhimu katika safari yake ya muziki. “Kaka yangu Lai alikua bega la kuanzia, alisaidia mimi na mchafuzy, hadi tukafika hapa,” alisema kwa upendo.
Kwa sasa, J Crack anajiandaa kutoa EP nyingine mwaka huu, na mashabiki wake wanategemea muziki wa kipekee kutoka kwake. “Muziki wangu ni kwa ajili ya shabiki, na EP yangu inayokuja itakuwa ya kipekee,” alisema.
Akihitimisha,ameweza kuwashukuru mashabiki hasa wale ambao wanafurahia Ep yake kwa kuonyesha upendo kupitia mitandao mbali mbali kwamba anawapenda sana.Ametoa shukrani za kipekee kwa wadada ambao wapo nchi za nje hasa Warabuni kwa kuiskuma Ep yake.