Nairobi, June 18- Msanii wa Hiphop na mwanaharakati wa muda wote ukanda wa pwani amewachana na kuwapa onyo mashabiki wanaomtukana kwenye mitandao.

Kupitia mtandao wake wa Facebook ameandika hivi;
“Onyo kwawanaonitukana:Acheni unafiki! Wakati nilikuwa nikiimba nyimbo za kuikosoa serikali, kupigania haki, na kuhamasisha jamii, hamkuwa mkiniunga mkono. Sauti yangu ilikuwa sauti ya wananchi — lakini mlikaa kimya, mkiangalia kwa mbali.

Sasa nimeamua kuchukua hatua zaidi, nimechagua kuingia kwenye siasa ili kuleta mabadiliko ya kweli kutoka ndani ya mfumo ghafla mmeamka, mnanza kunitukana?
Kumbukeni: Harakati si maneno tu, ni matendo. Nimechoka kuwa msemaji wa mabadiliko nikiwa jukwaani pekee. Sasa nafanya kazi ya kweli ya kuyasimamia yale tuliyokuwa tukiimba.
Kama huwezi kusherehekea hatua za maendeleo, basi usiwe wa kwanza kupiga mawe.

Kulingana na Chibo Dee ni kwamba ameamua kuingia kwenye siasa ili kuleta mabadiliko akiwa ndani kwani muda akiwa mwanaharakati, watu walimuangalia tu bila kumuunga mkono.

Haya yanajiri huku msanii huyo akiendelea na nia yake ya kwamba hatalegeza kamba kwa kufuata ndoto zake na mambo yake binafsi. Siku moja baada ya chapisho hilo,Chibo alimpost Mwakilishi wadi wa Tezo, Thomas Chengo na kumtaja kama kiongozi mchapa kazi katika kaunti ya Kilifi na kusema kwamba atakuwa anaenda hatamu tatu kwenye wadhfa huo. Chapisho hilo limefanya baadhi ya mashabiki kuhisi kwamba Chibo Dee atakuwa amebadilika kutoka kwa mwanaharakati hadi kwa chawa wa viongozi.

Msanii huyowa Hiphop amekuwa akionekana kwenye sherehe na shughuli za kiserikali za kaunti ya Kilifi kwa muda sasa huku baadhi ya mashabiki wakisema kwamba aendelee kuchapa kazi bora inamletea kipato wala asiskilize maneno ya watu kwenye mitandao.

Mwamba ameachilia kazi kadhaa za kiharakati na kuwa miongoni mwa wasanii ambao wanaisemea jamii.Hoja,damu ya Kenya na nyenginezo ni baadhi ya kazi zake za kiharakati.Amefanya kazi na Wasanii kama vile Tricks, Roy Billionaire, Susumila ambazo zimemfanya kujulikana zaidi mkoani.Sasa hivi anatamba na ngoma yake inayoitwa Mungu Kwanza.

Kulingana na maoni ya mwandishi, Chibo Dee yuko na haki ya kufuata anachokitaka yeye. Yuko na haki kama mkenya,kumuunga mkono kiongozi, mrengo anaoutaka yeye.Kuwa msanii na kioo cha jamii ama mwanaharakati haimaanishi kupinga tu kila kitu, unaweza ukawa mwanaharakati wa kupinga na pia wa kuunga mkono.


Maoni yako ni gani kuhusu Chibo Dee kuingia kwenye siasa hata baada ya kukemea wanasiasa?

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *