Mombasa, July 23- Kidis The Jembe ameendelea kuwa miongoni mwa wasanii wanaozua gumzo kila uchao kutokana na kauli zake na miradi yake ya kisanaa. Katika mahojiano ya hivi punde na Tizo The Presenter, msanii huyo alifichua kuwa ana kazi nyingi zinazokuja.

“Saa hii ni kazi juu ya kazi. Ulimuona dadangu Nyota ameenda. Niko na kazi na Tee Hits, Susumila, Batengo. Kuna verse pia nimetumia kakangu Diamond Platnumz. Mdogo wangu Byser naye pia tuna jambo,” alisema Kidis.

Kwa sasa, Kidis anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wenye nafasi nzuri ya kuendelea kutikisa katika sanaa, kutokana na jinsi jina lake limekuwa likitajwa mara kwa mara kwenye mitandao na vyombo vya habari.

Ngoma yake mpya, Ngoma Draw aliyomshirikisha Almasi, imepongezwa vikali na mchekeshaji maarufu kutoka Pwani, Magwaya Ndani, ambaye alimtaja Kidis kama msanii wa kipekee anayetoa kazi zinazovuma kila wakati.

Katika habari nyingine, Kidis ameendelea kumtetea Wakili George Kithi wiki chache baada ya picha kuzagaa mtandaoni zikimwonyesha akiwa na msanii kutoka Tanzania. George Kithi amekuwa akileta wasanii mbalimbali kutoka Tanzania kama Mbosso na Harmonize kuwaburudisha mashabiki katika matamasha ya kufunga mwaka kaunti ya Kilifi.

Kupitia mahojiano hayo, Kidis alisisitiza kuwa tatizo si wasanii wa nje, bali ni mfumo wa sanaa nchini.
“Akileta Mbosso sawa tu. Akitaka alete hata Chris Brown. Tunahitaji mfumo wa kufuatilia mziki wetu. Hii ni kuhusu monitoring system. Ni KSh 50 milioni Mheshimiwa, kama unaijua hiyo, nitafute,” alisema Kidis.

Pia, Kidis aliwajibu mashabiki waliomponda kwa kurudia mavazi. Alisema tofauti na baadhi ya wasanii wanaokodisha nguo kwa ajili ya kuonekana, yeye huvaa nguo zake mwenyewe.
“Nguo ni zangu. Nitavaa hadi nguo za ndani na niwaonyeshe jinsi ninavyozirudia. Mimi sivalii kufurahisha watu. Mvimbe mpasuke,” aliongeza kwa utani.

Aidha, aliwasihi wasanii wakongwe kama Nyota Ndogo, Susumila, P Day na wengineo wasikate tamaa bali waendelee kuachia kazi mpya na kuendeleza muziki wa Pwani.

Kwa sasa, Kidis anatamba na Ngoma Draw ambayo inafanya vizuri kwenye mitandao, ikifuatia mafanikio ya wimbo wake Bonge la Toto aliyomshirikisha Shabiggy.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *