Mombasa, Julai 25- Chama cha Mawakili nchini (LSK) tawi la Mombasa kimelaani vikali hatua ya Rais William Ruto kuanzisha ujenzi wa kanisa ndani ya Ikulu ya Nairobi.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee kwenye kipindi cha Mo Breakfast Club mapema leo, wakili Jackson Muchiri alisema kuwa sheria haimruhusu mtu binafsi kuanzisha miradi ya kibinafsi kwenye ardhi ya serikali. Alieleza kuwa hatua hiyo ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi.

Muchiri aliongeza kuwa ujenzi wa kanisa hilo si kipaumbele kwa sasa, hasa ikizingatiwa hali ngumu ya kiuchumi inayowakabili Wakenya wengi kwa sasa.

Aidha, alisisitiza kuwa Kenya haina dini rasmi ya serikali, na hivyo ujenzi huo unaweza kutafsiriwa kama ukiukaji wa misingi ya kikatiba, hususan kuhusu utenganisho wa dini na serikali.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *