Mombasa, Kenya, Januari 21- Mwana hiphop kutoka kaunti ya Mombasa ,Davy Gze ameweka wazi hali yake ya kiafya kwamba si nzuri.
Davy Gze amekuwa akichapisha kupitia mtandao wake facebook kwamba hayuko sawa na yuko hospitalini jambo ambalo asilimia kubwa ya mashabiki hawajaliamini hilo wakidhani kwamba anafanya kiki.
Davy Gze amekuwa miongoni mwa wasanii wenye kufanya matukio kabla kuachilia kazi zake.
Kabla ya kisa cha kulazwa, kulienea habari kwamba Gze kafumaniwa na mke wa mtu kisha badae ikajulikana ilikuwa mchezo tu.
Gze alikuwa amepost hivi kwenye facebook yake;
‘Ukweli ni kwamba wasanii wengi vifo vyao huchangiwa na watu wao wakaribu na mashabiki wao kutokana na kukosa msaada au maombi kutoka kwao kutokana na kuamini kila kitu msanii akipost ni Kiki. Mfano Mimi napitia hali ngumu sai ya kiafya ila unakuta mtu ananipigia simu ananiuliza ngoma mpya watoa lini ju nimeona umepost Kiki kwamba umelazwa hospitalini😳cha kusikitisha unakuta msanii mwenzako ndio anasambaza akisema ni kiki wakati ww upo umelazwa hospitalini unapigania uhai wako.’
Akizungumza kwenye The Rush Hour kwa njia ya simu, Jumatatu tarehe 20 Januari 2025, Gze amesema amelazwa hospitalini kwa anaugua homa na maumivu ya mwili mzima.
‘Niko hosii nimelazwa hapa sijui natoka lini lakini hali yangu si nzuri,inasikitisha kuona hata baadhi ya wasanii wananipigia simu kuniuliza natoa ngoma mpya lini.Kiukweli niko mgonjwa,’ amesema msanii huyo.
Ikumbukwe kwamba Dacy amefanya kazi na wasanii kama vile Chikuzee na Fisherman ikiwa ni ya hivi punde zaidi.
Msanii mwenza, Ziky Mtanah amejitokeza kumshauri Davy kutoeleza shida zake kwenye mitandao kwani wengine sio marafiki wa kweli. Ziky ameandika hivi kwenye facebook yake;
‘Duuh Davy Gze pole mwanangu. Yote maisha kaka mganga wa kweli Mungu kaka. Utapita pia hapa. Kitu nakushauri kaka kwa huu wakati unapitia punguza marafiki wasijue unachokipitia . Hakuna mtu mbaya kama rafiki. Punguza kuaniÄ·a shida zako mitandaoni . Huku mitandaoni iwe 10% ya maisha yako watu wasikuelewe . Utashinda . Usipelekwe na kelele za watu . Hii ni mitihani hata sisi tunapitia mdogo wangu .. Chagua marafiki kaka rafiki ni yule anakustiri hata akijua wewe ndo mkosa.’
Hivi unadhani hii ni kiki ama ni kweli?