Mombasa, March 11 – Mtayarishaji muziki maarufu na pia msanii kutoka kundi la Watu Wazim, Master Watu Wazim afunguka kuhusu gumzo linaloendelea kwenye mitandao kuhusu kuibiwa vyombo vyake vya studio.

Kulingana na Master, vyombo hivyo ambavyo vilikuwa kwenye nyumba yake ya mshomoroni kwamba viliibwa kama wiki zilizopita na msanii tajika.

Kupitia video kwenye mtandao wake wa facebook, Master amekanusha madai ya kuwa anafanya kiki kwani mashabiki wengi wa Ukanda wa pwani hudhani matukio ya wasanii huwa yamepangwa tu.

Master ameeleza kupitia video hiyo kwamba yeye na wasanii wa kundi la Jacugaz wamekuwa marafiki wa muda mrefu ila kwa hili hakuna urafiki.

Kickmaster anasema kuna muda msanii wa Jacugaz, Fareed hakuwa na makaazi maalum ndio akajitolea kumpatia chumba kwenye nyumba yake ya Mshomoroni ambayo pia ilikuwa na vyombo vya studio.

Akieleza, Master amesema kwamba Jacugaz alienda huko kama kawaida yake akafungua nyumba kama kawaida na kutoka na vyombo hivyo na tangu siku hiyo hajaonekana.

“Nimepiga ripoti polisi na niko na OB kwasababu baada ya kuambiwa ametoka na vyombo vyangu vya studio, nilienda mbio sana kwasababu nilikuwa nimepanic na kweli kufika sikuona vyombo vyangu ndio nikaenda kuripoti Concodia Police Station. Kuanzia hiyo siku, bado anatafutwa na pia namtafuta sijampata, tulienda kwao, Mamake akasema tangu siku ambayo alitoroka na vyombo vyangu kwao pia hajafika. Nimeamua kufanya video hii kuwatahadharisha tu, endapo utauziwa vitu vya studio nipigie ama ukaripoti kwa kituo cha polisi tunamtafuta,” amesema Master.

Habari hizi ziliwekwa usiku wa kuamkia leo na msanii Ashley Queen ambapo imezua gumzo baada ya mashabiki kuchukulia kama kiki.

Ashley aliweza kuandika hivi kupitia ukurasa wake wa Facebook; Hii ni tahadhari kwa wote, Kuna vyombo vya studio vilivyoibwa na mwizi anajulikana ,hivyo basi nakutaarifu usije ukauziwa vyombo hivyo manake vinaweza kukuweka kwenye matatizo hata wewe ulieyeuziwa. Mwizi wa vyombo hivyo Anaitwa Faridy Jacugas, kwa sasa ako mafichoni kwa kuwa anatatutwa na police. Endapo utamuona mtu huyo mahali popote tafadhali naomba utoe taarifa.

Msanii wa kundi hilo la Watu Wazim, Mfalme Moher ameweza kuingia kwenye comment section na kusema kwamba watu wanachukulia kiki jambo la kweli.

Kulingana na Katana, anasema walijua tu wakiweka kwenye mitandao watu watadhani ni matukio ya kupanga badala ya ukweli. Daddy Q ameonyesha kuskitishwa na jambo hilo kwa kulichukulia kama kiki.

Kufikia sasa, hakuna msanii yeyote kutoka kundi la Javcugaz ambaye amezungumza kuhusu suala hili.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *