Mombasa, Agosti 1- Msanii maarufu nchini, Johnny Skani, amezua mjadala mitandaoni baada ya kutoa maoni yake kuhusu hali ya sasa ya sanaa ya Pwani akiwajumuisha wasanii, madj, waigizaji na hata vyombo vya habari akisema mambo si kama zamani.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, aliandika ujumbe ufuatao:

“This goes out to Coast entertainment industry. Nikiandika hivi, labda mtaelewa.
You still have a long way to go. Bado. Bado. Bado.

All I see ni kalongolongo mingi inaendelea.
Kama mngekuwa wasikivu na wanyenyekevu, bila kupishana kwa vijembe, mambo yangekuwa tofauti.
Lakini uswazi mwingi umewalemaza.

Kwanza, muziki hakuna kabisa! Vitu naskia mwisho wake ni kwa disco matanga.
No proper branding, no serious marketing ni upuzi mtupu.
Wale wanaojiita wasanii wakubwa sasa hivi, jamani, wanahitaji darasa na maombi.
Maproducer wazuri walichoka. Waliobaki ni copy paste ya Bongo na hata Bongo yenyewe ilishapitwa.
Wote mnakimbiza clout, tena cheap sana.

Redio hadi zinafungwa!
Bloggers ni wachache wanaojitahidi, lakini inawabidi kubuni story feki ili mtambulike.
DJs wamebaki ku-survive na gigs za pen mbili kwa sababu waliwasahau wale waliowainua.
Event organisers walikimbia kiwanja, shida ikiwa ni mikopo na kuwakandamiza wasanii.

Hata models siku hizi ni kama warembo wa mtaani wanaojaribu kupamba video na kuonekana kwenye gigs.
Ukijaribu kuwaelekeza kidogo tu, wanakukasirikia.
Clubs zimekuwa uwanja wa mapambano madj wakipigania nafasi kama soko ya Kongowea.
Hakuna viwango!

Ujumbe wake umeungwa mkono na wadau mbalimbali wa sanaa akiwemo Steve Kipande maarufu kama Daddy Q, huku Levy The Don naye akiongeza kupitia mitandao ya kijamii:

“Nakusupport big brother Johnny Skani.
Entertainment industry ya Coast inahitaji maombi ya kweli kabisa.
Imejaa wanafiki, wadhulumaji na wachawi.
Tunahitaji mkesha wa wiki mbili tufukuze mapepo yote.”

Maoni yako ni yapi kuhusu hali ya sanaa ya Pwani kwa sasa?

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *