Mombasa, Septemba 10- Tamasha la sherehe za chenda chenda hufanyika kila mwaka tarehe 9 mwezi wa Tisa mambapo jamii ya Wamijekenda huungana pamoja kusherehekea tamaduni zao mbali mbali.Tamasha hili ambalo huwa linaongozwa na wazee wa Kaya.
Siku hii huwa ni ya shangwe, ngoma, nyimbo, maonyesho ya mavazi ya kitamaduni na maonyesho ya mikono (crafts) yanayoonyesha ustadi wa jamii hii ya kale.Kabila Tisa za Kimijikenda ambazo huhusika ni pamoja na Wagiryama, Waduruma, Wadigo, Wachonyi, Wakambe, Warabai, Wakambe, Wakauma na Wajibana.
Mara nyingi,sherehe hizi hufanyika Kaloleni,Rabai na maeneo mengine yaliyopendekezwa.
Chenda Chenda huwa na umuhimu mkubwa sana kwa Wamijikenda ikiwemo kuendeleza utamaduni kwa kuleta pamoja kabila zote tisa na kuonyesha baadhi ya tamaduni zao kama vile kusaga mahindi kwa kutumia jiwe, kutwanga kutumia kinu na mchi na mengineyo.
Vile vile chenda chenda huchangia kuleta umoja kwa kuleta watu pamoja na kutoa jukwaa kwa wasanii, wapiga ngoma na wazee kuonyesha asili na kujivunia tamaduni zao.
Sherehe hizi hutumika kama njia ya kuwarithisha vijana wa Kimijikenda kuweza kuijua zaidi lugha yao na tamaduni zao.
Mwaka huu,sherehe za chenda chenda zinafanyika sehemu mbili tofauti ambayo haijawahi kutokea.Sherehe zinaendelea Kilifi huku Kwale pia zikiendelea.Je kuna athari gani ya kuwa na mgawanyiko kwenye tamasha hili la kiasili.
Awali, Chenda Chenda Festival ilitangazwa kufanyika Kwale ambapo baada ya muda, Kilifi pia kukatangazwa kuwa na tamasha hilo hilo. Kupitia barua rasmi kwenye ukurasa wa Kaunti ya kilifi baada ya wazee wa kaya kuweka barua yao pia ya kupinga vikali sherehe hizo kufanyika mahali kwengine,barua Kilifi iliandikwa hivi:
Kwa sasa,sherehe hizo zinaendelea,moja inafanyika katika chuo kikuu cha Pwani kaunti ya Kilifi huku Kwale ikifanyika Kasemeni.
Je kuna athari yoyote ya kufanyika kwa sherehe mbili za chenda chenda kwa siku moja?