Mombasa, Septemba 17- Joseph Kai maarufu Presenter Kai ambaye anafanya vyema kwenye mitandao kupitia kazi zake ameweza kuandika kwa maskitiko makubwa kuhusu watu wanaotumia picha zake na mpenzi wake Diana vibaya.
Kai ameweza kuchapisha ‘screenshots’ za kijana anayeitwa Apollo Creatives kwenye mtandao wa Facebook na kudai kwamba amejaribu kumkanya ila hajaskia.Kai ameandika hivi,’Tunawapenda sana na kuwaheshimu mashabiki zetu ila sio kwa kutukosea heshima namna hii. Nimekuwa mngwana hata kumwambia awache ila hajasikia sasa wacha sheria imshughulikie. Hatutakubali kuharibiwa images putting in mind we represent so many companies. Ikawe funzo kwa watu wote’.
Ikumbukwe kwaamba sio mara ya kwanza watu kutumia picha zake na Diana vibaya,wengine wamekuwa wakitumia majina kujifanya kuwa Kai na kuwadhulumu wakenya.Miezi miwili iliyopita,yupo mtu aliyekuwa anatumia jina la Presenter Kai ambapo baada ya kupatikana,aliweza kuomba msamaha na akasemehewa.
Kulingana na baadhi ya mashabiki,wanamuunga mkono Kai kwamba aweze kuwachukulia hatua wanaomdhalilisha kwani watafanya mazoea huku wengine wakisema asamehe tu kwai hao pia wako katika harakati za kutafuta pesa.
Kwenye mtandao kama vile Facebook,Kai na Diana wameweza kuiteka na kuwa gumzo kila siku kupitia machapisho yao ya upendo na kuonyesha mapenzi.Kai na ‘my wife’ wameweza kupata biashara kupitia mitandao yao na kuwa na wafuasi wengi.Kwenye tafiti zangu,baadhi ya waunda maudhui wanaongoza pwani kwa wafuasi wengi,Presenter ni namba moja.
Ikumbukwe kwamba,mwamba alianza safari yake ya kutengeneza maudhui ya kuweka kwenye mitandao miaka michache iliyopita baada ya kuwa kwa redio kisha televisheni kwa muda.Sasa hivi Kai anaendela kuishi maisha yake kupitia mitandao na kuwadhirishia vijana wengine kwamba inawezekana.