Mombasa, November 19- Msanii wa Kike kutoka ukanda wa Pwani Esther Mwangala Mdzihana maarufu kama Adasa ameamua kufunga mwaka na Ep.

Adasa ambaye mwaka huu ameachilia kazi na Iddi Singer, ameendelea kuwa kwenye mioyo ya mashabiki wengi huku wakisubiri kazi hizo. Kupitia mitandao yake ya Kijamii,Adasa ametangaza kudondosha Ep inayoitwa Wira tarehe 22 mwezi huu wa Novemba,2024.

Wira ndio jina la Ep yenye nyimbo saba ambazo ni Mulungu akiwa na Bosco Baya, Mudzichenda ,Wira, Henzo akiwa na Iddi Singer, Mudzini akiwa na Kaa la Moto, Nirichika akiwa na Manu Bayaz na feeling So Good.

Kulingana na kipande kifupi cha video alizoweka,Wira ni muziki kwa lugha za kimijikenda na wengine huita ‘music’ kwa lugha ya kigeni, ishara ya kwamba huenda asilimia kubwa ya ngoma kwenye Ep zikawa kwa lugha ya kimijikenda.

Adasa hata hivyo atakuwa amepiga hatua nyengine zaidi kwa kuiw3akilisha sauti ya mtoto wa kike kwenye sanaa na muziki wa pwani.Ikumbukwe kwamba Adasa amefanya kolabo na wasanii tajika nchini akiwemo Khaligraph Jonees, Benzema, Stevo Simple Boy na wengineo. Amefanya kolabo na wasanii wengine kutoka hapa Pwani akiwemo Happy C, Manu Bayaz,Iddi Singer,Tee hits,Tricks na wengineo.

Ikumbukwe kwamba,Adasa ameshawahi kufunguka pia kupitia mahojiano ya simu kwenye kipindi chetu cha The Rush Hour kwamba anasomea muziki.Kulingana na maelezo yake wakati huo,alisema anasomea kucheza ala mbali mbali za muziki na mambo mengi yanayohusiana na muziki.

Kupitia mahojiano hayo hayo,Adasa hakufunguka kuhusu kuwa kwenye usimamizi mpya wala suala la mahusiano.Adasa amekuwa kwenye ramani na ngoma zake kama vile Nipekeche,Tunaendana,Nisepe,katika,Hatuachani na ngoma nyengine nyingi.

Amekuwa miongoni mwa wasanii wakike wanaotazamwa na kufuatiliwa kwa ukaribu pia na wasanii wachanga kwa lengo la kuwatia moyo na kuwaonyesha kwamba wanaweza.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *