Nairobi, Kenya, December 17- Wikendi iliyopita, kumekuwa na michuano ya fainali za kombe la Rashid Abdalla maarufu Rashid Abdalla SuperCup kaunti ya Kwale.Mbali na mpira ambao Denmark Fc waliweza kuchukua ubingwa,kulikuwa pia na burudani kutoka kwa wasanii mbali mbali ikiwemo Kelechi Africana, Kidis, Jay Melody na Nandy kutoka Tanzania.

Gumzo mtaani kwa sasa kuhusu msanii Kidis the Jembe ambaye amejipata kwenye midomo ya mashabiki baada ya kuingia Kwale na gari ya aian ya Range Rover yenye jina lake.Kwa haraka haraka tu, huenda ikawa gari hizi zimeandaliwa na wenye fainali ili kuwaheshimisha wasanii kwani sio jambo geni wasanii kuenda kwenye shughuli kubwa kama hizi na gari na misafara ya gari kubwa.

Mashabiki wameweza kumuingilia Kidis na kumwambia gari sio yake kupitia machapisho mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii. Ikumbukwe kwamba hakuna mahali popote ambapo msanii huyo alitangaza kuwa na gari.

Washikadau na wasanii wameweza kuonyesha kuskitishwa na aina ya mashabiki wanaoponda bidi za wasanii wa nyumbani. Susumila ameweza kumkingia kifua Kidis kwa kuandika hivi; Watu wanaongelea negative ni sababu they are bitter about themselves now wanaona wamtolee mwenzao negativity zao unapodiss msanii ambae anaishi ndoto zake anapush talent yake ili kufikia malengo yake ya kimaisha jiulize na wewe unaemponda umefanya mini kutimiza ndot zako ama malengo yako ya kimaisha?

Shirko pia amejitokez kumtetea Kidis kwamba mashabiki wenye chuki na wivu hawapendi wasanii wao. Kulingana na Shirko, wivu na chuki ambazo hazisaidii zikiondoka,Sanaa yetu itasonga mbele.

Hata hivyo, Kidis bado hajapost chochote kuhusu show yake ya juzi wala gumzo linaloendelea. Kulingana na mwandishi wa Makala haya, Kidis alifanya jambo kubwa la kufurahiwa na jambo ambalo linafaa mashabiki walipokee kwa uzuri. Labda upande ambao Kidis anafaa kuuzingatia ni upande wa mpangilio kabla kupanda kwa steji ikiwemo kujua ni ngoma gani itaannza na gani itafuata.

Akiwa jukwaani alionyesha wazi kwamba hakuwa na ushirikiano mzuri na dj haswaa kuhusu ni ngoma gani ambayo alifgaa kuanza nayo ama kumaliza nayo.Kuhusu kutumbuiza,alicheza sana muziki wakati mashabiki walimngojea muongozo wake. Yote Tisa, Kidis ni Jembe, wikendi imekuwa yake na kufanya wasanii kama vile Nandy na Jay melody wasiongelewe.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *