Mombasa, Kenya, October 15- Shirko Awadh Salim maarufu Shirko Media ambaye ni miongoni mwa watayarishaji muziki tajika na wenye tajriba kutoka Afrika Mashariki na pia vile vile msanii ameweza kufunguka mengi kuhusu safari yake kwenye sanaa.

Kupitia kipindi chetu cha Coastal Vybez siku ya Jumamosi 12 Oktoba, Shirko ameweza kufunguka kwamba kwa sasa Shirko media iko na ngoma nyingi ambazo zipo tayari bado kuzidondosha tu. Amejibu swali ambalo mashabiki wamekuwa wakijiuliza sana kuhusu ukimya wao licha ya kuwa na mafundi wa muziki kama vile Dazlah Kiduche na Ally Mahaba.

“Tulikaa kimya muda mrefu kwasababu tulikuwa tunajipanga na kurekodi ngoma nyingi…tutatoa ngoma nyingi nyingi hadi tupate moja ambayo itatambulisha identity ya Dazlah.Mbali na Dazlah na Ally Mahaba tuko na wasanii wengine sit ana wote wako na ngoma,” amesema Shirko.

Sio hayo tu, Shirko ameweza kufunguka kwamba juhudi zake zipo kwenye kuubadilisha muziki wa wasanii wake kulingana na wakati na kuachilia makombora yaliyo bora. Amesema walipeana muda wa wasanii wengine kutamba na kuachilia kazi zao lakini wanaona wasanii wengine hawakuweza sasa ni muda wa Shirko Media, hapatakalika kwani anaamini kilichopo jikoni kitairegesha heshima ya muziki hapa nchini.


Ameitaja ngoma ya Kidekide iliyotengenezwa na Tee Hits kwamba hata wakati huo bado Tee aliiga mfumo wale aliokuwa akiutumia na Yamoto Band kwenye kuunda biti za ngoma hiyo.

Ubinafsi na wivu wa washikadau mbali mbali wa sanaa,ameutaja kama njia mojawapo ya sanaa yetu kukosa Kwenda mbele. Hii ameilinganisha na heshima anayopewa nchini Tanzania kama mtayarishaji muziki ambayo ni tofauti na hapa pwani.

Shirko vile vile amesema kwamba watu wengi wanajua uwezo wa kuibeba sanaa ya pwani na kuifikisha mbali anao ila wanamuogopa wakidhania watakosa unga.Ikumbukwe kwamba Shirko ni miongoni mwa watayarishaji muziki wenye mafanikio makubwa na waliochangia kuvizindua na kuvipatia mwangaza vipaj vingi sana hasa Tanzania.

Awadh amefanya kazi na wasanii tajika ambao wamefanikiwa kupitia muziki kama vile Diamond Platinumz, ameilea Yamoto band, Berry Black na wengine wengi kama prodyuza na msanii vile vile.Ngoma ya hivi punde zaidi ikiwa ya Mboss inayoitwa Ova ambayo pia ameweza kuhusika pakubwa na kuongeza utamu kwenye ngoma hiyo. Akiwa Bongo kwa mkubwa na wanawe,amelea wasanii kama vile Rayvanny,Young Luny ana wengien ambao walikuwa wadogo enzi na sasa wako na majina.

Ticha Shirko amesema kwamba aliacha usanii kutokana na sababu nyingi tu iiwemo masuala ya familia.Anaendelea kuekeza knguvu zaidi kwenye utayarishaji muziki japo amesema watayarishaji muzki wengi wako na uwezo pia kuimba japo huiona kama kazi ngumu kwa kutayarisha muziki kuna raha yake ya kuongoaongoa wakati wa kuutengeza.

Hajalisaza suala la wasanii Akeelah na Sai Kenya ambao walikuwa kweye mikono yake.Kulingana na Shirko,hajawahi taka mtu akose kutimiza ndoto zake wala yeye kuwa kizuizi cha talanta ya mtu ila wakati mwengine inabidi.


Kuhusu Sai kenya ni kwamba baada ya kuingia kwenye ndoa halali,mumewe alitaka kuwa msimamizi wa kipaji cha mke wake ambapo kulikuwa na ugawaji wa majuku kati ya mumewe na Shirko Media.Salim amesema kupitia ndoa yao na mabadiliko ayo,mume wa Sai hakutaka mkewe afanye video na mwanaume yeyote yule kwasababu ya wivu ambapo hii iliongeza ugumu wa kazi kwa pande zote mbili.

Yote tisa, kumi ni kwamba uongozi wa Shirko media umetangaza kuachilia balaa kuanzia mwaka huu na kuahidi kwamba hakutakalika.Wanasema ni mwendo wa ngoma baada ya ngoma kama Wasafi wanavyofanya.


Kama unawakubali Shirko Media basi endelea kuskiliza ngoma zao kupitia Mo radio 88.2fm kila siku.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *