Nairobi, Kenya, January 15- Nyota Ndogo ni msanii maarufu wa muziki kutoka humku nchini. Anajulikana zaidi kwa sauti yake tamu na uwezo wake wa kuimba katika muziki wa taarab, ingawa ameweza pia kujipatia umaarufu katika nyimbo za muziki wenye asili ya kipwani ambao umempatia maarufu kote Afrika Masharikii.
Nyota ambaye alizaliwa kaunti ya Taita Taveta,alianza safari yake ya muziki akiwa na umri mdogo hadi sasa.Amekuwa miongoni mwa mastaa wa kike kutoka humu nchini wanaofanya vyema kwenye soko la muiki.
Mwadada huyo ambaye amejikita kwenye masuala ya biashara mbali mbali Pamoja na upishi,amepata wafuasi wengi kupitia mitandao kama vile facebook kupitia maudhui yake anayochapisha kila siku.Kulingana na kurasa zake za kijamii,Nyota anapenda kuwa muwazi na kuzungumzia kila kitu ambacho hakiendi sawa.
Kwenye chapisho lake la hivi punde zaidi,Nyota amezua gumzo huku mashabiki wengi wakimuunga mkono kwa kauli yake ya kibishi.Ameandika hivi;Bora nipewe sura mbaya kuliko kunyimwa akili.atleast sura tutajidanganya na make up kujipa moyo ila akili ndioo hivyo sasa hovyo hovyo kabisa.
Kulingana na maoni ya mashabiki,kuna baadhi yao wenye humkejeli na kumuongelea vibaya jambo ambalo si saw ana halimyumbishi Nyota Ndogo.Nyota ni mwanamke anayejikubali ndio maana anakubalika.
Ikumbukwe kwamba mbali na kuwa hodari na mbunifu kwenye mitandao,Nyota vile vile anajihusisha na Nyota Jikoni ambayo ni biashara ya kuuza chakula.Ametengeza pia pilipili zake ambazo zipo madukani,anaendelea kufanya kazi na kampuni mbali mbali ikiwemo za unga na nyenginezo.
Nyota Ndogo pia aliweza kuskuma mbele tamasha alilofaa kufanya mwezi Februari kutokana na mjengo wake unaoendelea.Tamasha hilo lilikuwa limepangwa kufanyika mwezi ujao na wasanii kama vile Kidis,Chikuzee,dogo Richie ni miongoni mwa wasanii waliofaa kutumbuiza.