Mombasa, Januari 28- Mchekeshaji maarufu nchini, Ali Mwayogwe, maarufu kama Shugaboy, anaendelea kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii kupitia video zake zinazoteka hisia za wafuasi wake. Shugaboy, msanii mwenye kipaji kutoka Pwani, amekuwa kwenye midomo ya mashabiki kutokana na simulizi zake za ndoto za kushangaza ambazo, kwa mujibu wake, zimekuwa zikimkosesha usingizi.
“Nililala vizuri mara ya mwisho siku ya Boxing Day, lakini tangu wakati huo sijawahi kupata usingizi. Usiku naota nikiwaona marehemu kama Karisa Maitha, Ally B, na Mekatilili wa Menza wakinijia kwa ndoto.”
Hata baada ya kufunga na kuomba ili ndoto hizo ziishe, Shugaboy anasema mizimu imempatia masharti magumu mapya. Ameeleza kuwa amepewa jukumu la kufufua sanaa ya Pwani kwa sababu, kwa maoni ya mizimu, wasanii wa Pwani wameacha utambulisho wao na kuiga tamaduni za Tanzania.
Kuhusu sharti la tatu, Shugaboy alisema, “Hii ndio ngumu zaidi. Mizimu imenitaka niwanunulie magari Kelechi Afrikana na Dogo Richie ambao wamekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu lakini bado wanatembea kama ng’ombe. Sasa mshahara wangu wa elfu 70, nitaweza kweli?”
Kulingana na mchekeshaji huyo,watu walioaga dunia wanamkujia na kumuuliza maswali kuhusu sanaa ya pwani na kumtaka yeye aweze kuifufua.
Akizungumza kwenye video yake,Bwize anasema mizimu hiyo humpeleka msituni ambapo wanafanya mambo yao huko. Wasanii ambao aliwataja kama wakombozi wa sanaa ya pwani ni Pamoja na Susumila, Nyota Ndogo, Chikuzee na Masauti.
Hata hivyo, msanii huyo amefanya video nyengine mapema leo ambayo ametaja masharti magumu ambayo anasema amepewa upya licha ya yeye kujaribu kufunga na kuomba ili mambo hayo yamuondokee ila wapi.
Shugaboy,amesema amepewa kazi ya kuifufua sanaa ya pwani kwani wasanii wamekuwa wakizungumza Kiswahili cha nchi Jirani ya Tanzania Pamoja na kufanya wanachofanya watanzania ndio maana muziki wa pwani umeshindwa kujulikana kitaifa.Kwenye video hiyo,amesema amepewa masharti matatu ambayo anasema akikosa kufanya basi huenda akapotea tu kama msanii Czars alivyopotea.
Shugaboy alitaja masharti matatu aliyopokea:
- Kushirikisha Echo254 na Oga Obinna kwenye kolabo ndani ya siku 33.
- Kuandaa tamasha kubwa litakalojumuisha wasanii wote maarufu wa Pwani.
- Kununulia magari wasanii Kelechi Afrikana na Dogo Richie ndani ya siku 33.
“Nimeambiwa kuna wasanii kama Kelechi Afrkana na Dogo Richie am,bao wamekuwa kwa muziki kwa muda mrefu nab ado wanatembea kama ng’ombe, niwanunulie magari,sasa mshahara wangu wa elfu sabini, nitaweza kweli kuwanunulia magari? Na nisipofanya hivyo napotea sijui nitapeleklwa nchini gani” amesema Shugaboy.
Asilimia kubwa ya mashabiki wanahisi ni uchekeshaji anafanya tu huku akipitisha ujumbe kwa wasanii huku wakiwa na matarajio ya tamasha kubwa hivi karibuni ukanda wa pwani.Mashabiki wengine pia kupitia maoni kwenye mitandao mbali mbali, wanahisi huenda ikawa ni mambo ya kweli anayoyasema ya kuoteshwa huku wakimpatia ushauri wa kutafuta waombezi kwa hali anayopitia.
Asilimia chache wakisema ni malipo ya ‘wrong number anayoifanya kwenye kipindi cha redio kwamba huenda mambo yanamrudia.
Baadhi ya wasanii wengine ambao Shugaboy hajawataja,wamehisi kuvunjwa moyo kutokana na kauli za Shugaboy.
Ziky Mtanah ni miongoni mwa wasanii ambao walizungumza kuhusu kukatisha tamaa wasanii wadogo ambao bado wanajitafuta na kumuomba Shugaboy kusaidia kulea vipaji na sio kuvikatisha tamaa.
Hivi unadhani anachekeha ama mambo kama haya yapo?