Mombasa, Februari 13- Msanii wa muda mrefu kutoka ukanda wa Pwani, Happy C ambaye alipata umaarufu kwa zaidi ya mika kumi iliyopita akifanya kazi na kakake SD kwenye kundi la Wawindaji.

Wawindaji ni miongoni mwa makundi ya wasanii ukanda wa pwani yamekuwa yakitesa kupitia ngoma zao kama vile Christina, Morale na ngoma nyengine kibao.


Happy C alionekana kufanya kazi kama msanii wa kujisimamia baada ya aliyekuwa Gavana wa Mombasa, mheshimiwa Joho kuamua kumshika mkono Happy C.

Kupitia 001 Music, Happy C amefanya kazi kibao ambazo ni kuanzia Sema, Chekucheku na nyenginezo. Kumpitia mheshimiwa Joho, Happy C ameweza kupeta na kuonekana mwenye mafanikio kimuziki.
Mr Uptown kupitia mahojiano kwa njia ya simu kwenye kipindi cha The Rush Hour siku ya Jumatano tarehe 13 ambapo alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa,ameweza kufunguka kwamba sasa hivi yuko na wasimamizi wanne ambao wote ni kwa ajili ya biashara yake ya muziki.


“Niko na managers wanne,sitaki kuwataja saa hii lakini nitakuwa nawatambulisha rasmi, sitaki kusema Mwaringah anafanya kazi gani ila nitawatambulisha wote,” amesema Happy C kwa njia ya simu.


Msanii huyo amesisitiza umuhiumu wa kuwa na timu ya watu wanaokusaidia kufanya biashara ya muziki ambapo kauli yake ni sawa na ile Nasha Travis kwamba ni rahisi msanii akiwa na watu wanaomsaidia kwenye kuskuma muziki wake.


Uptown Pigo hajaishia hapo amezungumza kuhusu kurithisha kipaji cha usanii katika familia yake. Happy c amemtaja mtoto wake wa kiume kama watoto wenye kipaji kikubwa sna cha kuimba hii ni baada ya Happy C kumpost kijana wake mdogo akiimba wimbo wa Jay Melody wiki chache zilizopita.


Vile vile amesema nyumbani kwake anaskiliza ngoma zote na mtoto wake anajua ngoma zake pia kiasi kwamba akiwekea biti anaweza akaimba ngoma nzima.


“Nilijua kitambo sana kwamba mtoto wangu ana talent ya kuimba kwasababu huwa akiimba namrekodi,ni vile tu sikuwa napost.Haimbi ngoma za bongo pekeake kwanza anajua ngoma zangu pia na kuna ngoma nyengine hata nikuekea biti tu anaweza imba wimbo wote,” asema Happy C.


Jambo ambalo limewashangaza wengi ni kuhusu kauli ya msanii huyo kusema kwamba hawezi kubali mtoto wake wa kischana afanye muziki. Happy C hajaeleza sababu za kwa nini hataki ila amesema hata yeye yuko na kipaji na huwa anamchukua video ila hajawahi kuzianika kwenye mitandao.


“Siwezi kubali mtoto wangu wa kike afanye muziki hivyo tu, huyu wa kiume sina shida atafanya muziki japo sasa hivi nataka asome kwanza,” amesema Happy C.


Hivi unadhani kwanini wasanii wengi hawataki watoto wao wakike wafanye muziki?

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *