Nairobi, Agosti 26-Shabiggy ambaye pia anajiita Jeno The Don ameweza kufunguka mengi kuhusu sanaa yake.Shabiggy ambaye ni miongoni mwa mastaa na malejendari ambao wamekuwa kwenye sanaa kwa muda mrefu sasa hivi,ameweza kuzungumza kuhusu kazi yake mpya aliyomshirikisha Escobar Babake inayoitwa ‘watoto wa Mungu.’
Kupitia mahojiano ya Kipeke na mwanahabari wetu Yugebwize hapa Mo radio,Jeno ameweza kufunguka kwamba wako na ngoma nyingi tu ambazo amefanya na Esco ambazo wanaendelea kuziachilia.Kulingana na Biggy,album yao waliyoahidi kudondosha tangu mwaka jana,ndio hiyo ambayo wanaachilia wimbo mmoja mmoja.Kufikia sasa,Watoto Wa Mungu ndio ngoma yao mpya ambayo inapatikana kwenye mitandao yote ya kuuzia muziki.
Shabiggy ameisifia kazi yao mpya na kusema kwamba hakuna ngoma kali muda ukanda wa pwani kama yao.
Jeno The Don vile vile amezungumza kuhusu utofauti uliokuwepo kati yake ya Kidis the Jembe na kufunguka kwamba hawajazungumza kwa muda mrefu licha ya wao kuachilia ngoma kali pamoja mwaka jana.
‘Ni kapindi joh kuogea na Kidis,’amesema Kidis huku akisema hakuna sababu maalumu ya mazungumzo ya urafiki kati yao kukatika.Swala hili kwa mashabiki,walidhani labda ni kiki ila kulingana na Shabiggy,haikuwa kiki bali mambo ya kweli
‘Mimi si mtu wa kiki,sijafanya kiki.Usimpigie Kidis kwasababu itakuwa ni kutafuta lawama.’
Msanii huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii ambao wametoa ngoma kali kibao pia kupitia kolabo za wasanii kama vile Mchafuzy wa Mapozi,Esco,Kidis na wengineo,amepinga kauli ya wasanii kuhusisha sanaa na uchawi.
Mara kwa mara,kumekuwa na kauli kwamba wasanii wa pwani wanarogana.Kulingana na shabiggy kuhusu suala la uchawi kwanza amesema haliamini ila ameongezea kwamba kwa wanaoamini,basi uchawi upo.
‘Siamini kwenye uchawi manake mimi ni mtoto wa Mungu ila kwa wale ambao wanaamini kwamba kuna uchawi basi upo.’am,ejibu hukuu akicheka.
Baadhi ya vitu vya kawaida ambavyo watu hawavijui kuhusu msanii huyu ni pamoja na chakula ambacho anakipenda sana licha ya kushindwa kukipika mwenyewe,chapati maharagwe ndio chakula chake pendwa.Jeno vile vile mbali na muziki,hupenda sana utani na kufanya vituko vya kuvunja mbavu hasa kwa mashabiki wake.