Mombasa, March 19- Kaa La Moto ameandika ujumbe mrefu kupitia ukurasa wake wa Facebook kuhamasisha wasanii. Kaa La Moto ni miongoni mwa wasanii wa hiphop kutoka Afrika Mashariki, ambaye amekuwa akiwakilisha Swahili hiphop.

Ameandaa matamasha kama Burudani Experience kama njia ya kukuza vipaji na kuleta umoja katika sanaa.

Katika picha aliyoandika, Kaa La Moto alionekana na baadhi ya wasanii wa hiphop kutoka ukanda wa pwani. Picha hii ilisababisha gumzo, huku baadhi ya wasanii wakihisi kuachwa nje. Kaa La Moto alijibu kwa kusema: Tufanyeni Sanaa, Na Sio Kuwa Walimu Wa Sanaa!

Kumbuka kwamba sanaa na biashara ni vitu viwili tofauti. Unaweza kuwa mkali katika kutengeneza sanaa, lakini usiwe mkali katika kuisukuma sanaa hiyo mbele. Kinachojalika ni mtu kutoa mawazo yake na kuyaweka kwenye sanaa, siyo sana umekaaje kwa beat au style yako ikoje. Kuna watu wako off beat lakini wanapata mafanikio.

Unaweza kuwa na uwezo wa kufanya show nzuri, lakini ukakosa ushawishi wa kufanya watu wakutafute na kukuzingatia zaidi kwenye majukwaa ya kidijitali. Angalizo, discipline itakufikisha mbali zaidi kuliko talent pekee.

Kuhusiana na Wasanii wa Pwani
Ninaheshimu na kutambua wasanii wa hiphop kutoka Pwani, wakiwemo wasanii wa zamani na wapya. Wapo wengi zaidi ya 1,000. Natoa heshima kwa wasanii wote, wakiwemo waasisi, legends, wasanii wa zama yangu, na hata wale wapya. Pia nawajua na kuwaheshimu rappers wakubwa na wadogo wanaowakilisha Pwani ndani na nje ya miji.

Ninapotazama tasnia, napenda kukumbuka zama za Hip-hop Thursday Freestyle pale Pwani FM, na Hip-hop Teketeke. Pia, nilikuwa na tabia ya kutembelea maskani kutoka Lamu hadi Lunga Lunga, Voi, na miji mingine. Tumejenga upendo wa kweli.


Sanaa Kama Biashara
Sanaa pia ni biashara kubwa, na wapo wanaojituma tunawaona. Wengine wanajitahidi ili wapate heshima kwa mtaa, wengine wanataka kipato, na wapo wanaotaka kutambulika ili waonyeshe kwa wahuni au mademu. Wengine wanategemea familia zao, na wameshapita kwenye ile hatua ya sifa tupu bila mafanikio ya kifedha.

Hakuna sehemu imeandikwa kuwa kila msanii atapata nafasi mara moja. Kila biashara ina sheria na nafasi yake. Hii haimaanishi kuwa kama hujapata nafasi, basi wewe si bora. Ubora wa msanii unajulikana na yeye mwenyewe pamoja na timu yake.

Moyo wa Umoja na Kutambua Kila Mtu
Nina marafiki wengi, na sijawahi kuamini katika chuki au ushindani. Najua umuhimu wa umoja na kuleta watu pamoja ili sote tupate mafanikio. Ikiwa itatokea kuwa adui yako, hakikisha unajua tatizo lako. Katika miaka yangu mingi kwenye sanaa, nimeshuhudia watu wengi wa aina hiyo, lakini bado nipo na wao na wanajua hilo.

Kushirikiana na Wasanii wa Nchi Nyingine
Kumbuka, sanaa zetu hazina mipaka. Wasanii wa mataifa mengine wanaweza kuleta maono tofauti. Kama mtu akifanya kazi na wasanii wa mataifa mengine, wengine wanasema ameamua kuacha kushirikiana na wa nyumbani, lakini hiyo si kweli. Tuache kukosoa na kujifunza kushukuru hata kile kidogo mtu anachofanya, hasa kama wewe huwezi kufanya.

Subira na Kufikia Mafanikio
Mitandao inaweza kupotosha na kuonyesha hisia za kila mtu, lakini tusijitahidi kujudgiana kwa haraka. Heshima kwa kila mmoja ni muhimu. Subira ni muhimu kwa mafanikio. Kadri tunavyosubiri, ndivyo mambo yatakavyokuja. Najua kila mtu anahitaji kupata kile anachostahili, na sisi sote tuna nafasi ya kufika mbali.


Heshimu na endelea kuunga mkono wale unaowapenda, lakini isikufanye kuwa na kiburi au kuharibu biashara za wengine. Stick to your lane 💯
Ameandika, Kaa La Moto.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *