Mombasa, Septemba 10 – Huku sakata la wasanii wa Tanzania kutosaidia kusambaza kazi ambazo wanafanya na wakenya likiendelea kwenye mitandao,msanii wa Kaya Records,Dogo Richy ameamua kufunguka kuhusu changamoto alizopitia kwenye kolabo zake na wabongo.
Binladen kupitia ukurasa wake wa Facebook, amefunguka kwamba watanzania wamekuwa wakichukulia poa tu na hawana ushirikiano. Dogo Richy ameandika hivi;
Nimeona mnavyoandika na caption zenu nizakugonganisha watu mimi binafsi nimekuwa victim wa Hawa wabongo nishafanya nyimbo na beka flavor Hadithi na mpka kipindi hicho na tulipoteza hela nyingi sana juu tulienda mpka bongo kwa ajili ya kuandaa video na msanii akataka kututapeli Soo nilipoona na ukumbuka hakuwahi post hio nyimbo,thus nilipoona inahappen kwa mdogo wangu niliskia uchungu juu mm pia yamenikuta nikasema hawa wabongo mnawashobokea nn juu mm nimefanya ngoma mpka na tommy flavor na bado ctaki kuitoa na Wala sidhani kama nitaitoa juu ya kuvimbiana any way hapa bado tuna push ngoma ya kaka mdogo na tunavyoiongelea pia ni promo of which mm mwenyewe napenda
But respect sana kwangu mm c wajana nimefanya vitu mingi Sana Sina wivu huo wakijinga na msiongee tu share kazi yake juu pia mm nimeshare hapo chini
Kulingana na msanii huyo wa kizazi kipya, watanzania ni wagumu sana kwenye kusaidia kusambaza kazi za wasanii kutoka humu nchini.Ikumbukwe kwamba Richy Ree amefanya kolabo na wasanii kama vile Sam Wa Ukweli, Abdul Kiba, Beka Flavour na sasa anasema kolabo yake na Tommy Flavour ipo japo huenda isitoke.
Haya yanajiri huku Jimbi akizidi kuchekwa kisa amefanya kazi na Mr blue na Byser hajaweza kuisambaza kazi hiyo. Kulingana na washikadau mbali mbali wa burudani wanaendelea kusisitiza kwamba Mr Blue hafai kubebeshwa lawama kwani anafanya muziki kama biashara sio mambo ya kulazimishana.
Kwa sasa ngoma ya K.O aliyomshirikisha Mr Blue inaendelea kufanya vyema.
Ikumbukwe kwamba Nasha travis ameachilia ngoma mpya akiwa na Tommy Flavour hivi karibuni.Je Tommy ameshare kazi hiyo?Je kuna lazima ya wasanii wetu kufanya kolabo na watanzania?Je unadhani kipi kinafaa kufanywa ili kuepeuka changamoto hii?