Mombasa, Kenya, November 20- Msanii wa Kaya Records Francis Kalama maarufu kama Dogo Richie ambaye yuko na zaidi ya miaka kumi kwenye sanaa, amedokezea kutaka kubadilisha jina lake ambalo limemtambulisha kwenye muziki na kumueka kwenye ramani hadi sasa.
Dogo Richie kupitia mtandao wake wa Facebook, ameweka picha yake ya zamani na kuandika hivi, “Enzi hizo nilipokuwa handsom kabla sijavurugwa, naona si vibaya tukitumia Richie Ree badala ya Dogo Richie ama mwasemaje?Watu wanacomplain sana, mimi nahesabu kura wale wanataka nibaki Dogo Richie wacomment Dogo Richie wale wengione wacomment Richie Ree.”
Kupitia chapisho hilo,mashabiki wanaendelea kuweka maoni yao na kulingana na jicho letu la tatu, asilimia 70 ya maoni kwenye ukurasa wake, wanasema abaki kuwa Dogo Richie tu kwani wamemjua kupitia jina hil tangu zamani.
Mashabiki wengineo wameandika hivi:
“Mimi kama fan wako kutoka Taita Taveta nasema ibaki ivo ivo Dogo Richie, ndiyo tumekuita nayo since 2010 aisee…kama utaongeza mengine ongeza tu lakini ilo la Dogo usigusee.”
‘“Dogo Richy mpango mzima jomba.” – Rama Kahindi
Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki kupitia mtandao wake, huku wachache wakisema afanye kama alivyofanya Dogo Aslay hadi Aslay.
Ikumbukwe kwamba bado wasanii wanajiita Dogo ama Young hata wakizeeka. Dogo Janja kutoka Bongo, Young Killer, Young Lunya, Young Thug na wengineo, wamekuwa watu wazima ila bado wanaendeleza majina yale yale yao.
Ikumbukwe ni juzi tu Dogo richie aliweka kwenye mtandao wake jinsi anavyojivunia jina lake baada ya watu kutoka maeneo mbali mbali kujibatiza na kujiita ‘Dogo Richie.’
Hii inaashiria kwamba jina limemtengenezea mazingira mazuri ambapo anatambulika na kupendwa na mashabiki kuliko wasanii wengine ukanda wa pwani.
Dogo Richie kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Nimeachwa aliomshirikisha Masauti na Trio Mio na unaendelea kufanya vizuri kwenye mitandao.
Huenda akaachilia kazi nyengine kabla mwaka kuisha ila itakumbukwa kwamba msanii huyo amefanya kazi kubwa huu mwaka pamoja na kolabo kubwa na wasanii tajika ikiwemo Mr Seed.