Mombasa, Septemba 17- Sanaa mara nyingi asilimia kubwa ya wasanii huwa wa jinsia ya kiume huku jinsia ya kike ikiwa na wasanii kidogo. Pwani ni miongoni mwa maeneo yenye talanta nyingi pia za mtoto wa kike.Sauti, uandishi, uigizaji na hata masuala ya michezo, wapo wasichana ambao wanaiwakilisha pwani kila upande.

Pwani imeweza kutoa vipaji kibao huku baadhi ya wasanii waliopatia heshima toka zamani wakiwa pamoja na Nyota Ndogo, Mummy Dee, Confuser Jay, Jovial, huku wakina Adasa,Akeelah,Sai Kenya,Nana Kenya, Nasha Travis, Shanariha Evans, Wiwi Nimo, Wuddah Ann, Morinta, Mishy beib, Recho Shakes na wengine wengi.

Sasa hivi,wapo ambao wanaendelea kuzua gumz na kuzungumziwa zaidi kati ya hao ambapo ni pamoja na Shanariha Evans, msichana mwenye umri mdogo zaidi kwenye sanaa ukanda wa Pwani japo anafanya vyema.

Shanariha ameweza kupiga hatua kwa kuizunguka dunia kupitia muziki wake. Msanii kwa sasa ameweka histora mpya baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza kupitia ukurasa wa Dj AG Online jijini London. Nafasi hii ambayo Shanariha ameitumia, sio rahisi na hiyo imemfanya kuwa msanii wakwanza wa kike kutoka Afrika Mashariki kutumbuiza na pia baada ya Bien yeye ndio wa pili humu nchini kupata nafasi hiyo ambayo pia Diamond Platinumz aliweza kupata.Jukwaa la Dj AG wengi wamelitamani japo hawajafika.

Msanii wa Pili anayefanya vizuri kutoka pwani ni Mishy Beyb.Kupitia mahojiano na Mo radio wiki iliyopita, Mishy aliweka wazi kwamba video zake zimemgharimu sana na zina ubora wa kipekee.Ngoma yake ya Kiama ya hivi karibuni zaidi imemgharimu zaidi ya Laki Tatu ambapo bajeti yake inaingia kwenye bajeti kubwa ambazo wasanii kutoka pwani wamewahi kutumia na kuekieza kwenye kazi zao.Mashairi yake hayana mfano na hivyo basi kuwa miongoni mwa wasanbii wazuri ambao wanafanya kazi ya zaidi.

Nasha Travis anaendelea kukua kwa kasi zaidi. Chini ya miaka mitano, Nasha ameweza kujiongeza na kuonyesha muendelezo wa muziki wake.Ameongeza ubora kwenye uandishi,sauti pamoja na video zake pia. Nasha Travis ndio msanii wa kwanza wa muda huu kutoka Pwani kufanya kolabo mbili za nje kufikia sasa.Nasha ameweza kumshirikisha Barnaba Classic kisha akafanya kazi na Tommy Flavour ambayo inaendelea kufanya vyema kwa sasa.

Recho Shakes ni msanii wa nne ambaye amebarikiwa na kipaji na ana uwezi mkubwa sana.Shakes ambaye anapanga kuachilia dubwasha jipya hivi karibuni,ameonekana kutokuwa na kiu ya kutoka haraka ila anawekeza nguvu kwenye kazi zake.

Wapo wasanii wengine kama vile Wuddah Ann, Wiwi Nimo, Nanah kenya na wengineo ambao wanaendelea kuteka anga.Hawa ni baadhi tu ya wasanii wakike ambao leo tumewaulika japo wapo wengi ambao wanafanya vyema.


Msanii gani ungependa tumuangazie zaidi?

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *