Mombasa, Januari 30- Kundi la wasaniiwanaokua kwa kasi zaidi Pwani limeweza kuzua gumzo baada ya kubadilisha jina lao.Double Gang waliojulikana kupitia ngoma zao kama vile Anita,Maisha ya Ukweli na nyenginezo wamebadilisha jina.

Double Gang ni kundi la wasanii watatu ambao ni kamanda Pedeshee,kamanda Bushi na Kamanda Brown ambao kwa sasa wako chini ya ulezi wa Kubwa studios.

Je kubadilisha jina kuna athari gani kwa msanii ama wasanii? Hizi ndio baadhi ya changamoto ambazo huenda msanii akapatana nazo baada ya kubadilisha jina.

Kubadilisha jina la kundi la wasanii kunaweza kuleta athari hasa pale ambapo jina la awali tayari lilikuwa limeanza kujijengea nafasi kwenye soko la muziki. Jina la msanii ni sehemu ya utambulisho wa brand, na mashabiki hulizoea kulihusisha moja kwa moja na muziki, taswira na mafanikio ya msanii husika.

Msanii au kundi linapobadilisha jina ghafla, kuna hatari ya kupoteza muunganiko huo wa kihisia na kibiashara uliokuwa umeanza kujengwa, hali inayoweza kufanya baadhi ya mashabiki washindwe kuwatambua au kuendelea kuwafuata chini ya jina jipya.

Athari nyingine ya kubadilisha jina ni kuchanganyikiwa kwa soko na hadhira. Katika zama za mitandao ya kijamii na majukwaa ya kusikiliza muziki, jina ndilo linalorahisisha utafutaji, kufuatilia na kutambua kazi za msanii.
Jina jipya linaweza kufanya kazi za awali zipotee kwenye kumbukumbu za haraka za wasikilizaji, na hata kuathiri takwimu za streams, views na ushawishi wa kidijitali.
Kwa makundi yanayochipuka kama Double Gang, ambao tayari walikuwa wanaanza kutambulika, kubadilisha jina kuwa Makamanda kunaweza kuwafanya waanze upya mchakato wa kujitambulisha badala ya kujenga juu ya msingi waliokwisha uunda.

Japo kubadilisha jina huwa na athari kama hizo,wapo wasanii ambao wamaebadilisha majina yao na yamekubalika baada ya muda flani.Susumila ambaye anaendelea kutamba sasa hivi,alikuwa akijiita Kanali kipindi akiwa kwenye kundi lake na Escober Babake.

Cannibal amebadilisha na kujiita Chosen One,Aslay kutoka kwa dogo Aslay,Maromboso hadi Mbosso,Rabbit hadi King Kaka,yupo pia Chapatizo ambaye anajiita Tizo Bizness.Hii inaashiria kwamba huenda ikachukua muda ila watu watazoea na kazi zitaendelea kama awali.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *