Nairobi, March 5- Gumzo linazidi kuendelea kuhusu Marioo, msanii maarufu kutoka Tanzania, baada ya Tamasha la Tuzo za Trace lililofanyika Zanzibar mwezi uliopita.


Tamasha hili lilivutia umati mkubwa wa mashabiki, ambapo wasanii wengi walikabidhiwa tuzo, ikiwa ni pamoja na Bien, ambaye alishinda Tuzo ya Msanii Bora kutoka Afrika Mashariki. Licha ya tuzo hizo, kulikuwa na maonyesho ya ‘live performances’ kutoka kwa wasanii mbalimbali, ambapo Marioo alifanya onyesho ambalo halikufanya vizuri.

Kwa mujibu wa taarifa, Marioo, ambaye anajulikana kwa majina ya Omari Mohamed Mwamba, alikumbwa na changamoto ya kiteknolojia wakati wa onyesho lake. Mashabiki walikuwa na matarajio makubwa kutoka kwa Marioo, lakini walishangaa kuona msanii huyo akishindwa kuimba vizuri.


Katika mitandao ya kijamii, wengi walieleza kuwa walivunjwa moyo na jinsi onyesho hilo lilivyokuwa, wakijua kuwa Marioo amepata umaarufu mkubwa kutokana na nyimbo zake maarufu, ikiwa ni pamoja na hit yake Nairobi, aliloshirikiana na Bien.

Hadi sasa, Marioo hajaongelea suala hili wala kutoa ufafanuzi kuhusu changamoto aliyopitia. Hata hivyo, Mwijaku, ambaye ni mwanahabari na mtangazaji, ameibuka kumtetea Marioo. Katika mahojiano yake na Wasafi, Mwijaku amesema kuwa tatizo lililotokea ni kwamba Trace Awards hawakuwa na usawa kwa wasanii. “Trace Awards hawakuwa fair, ndio maana Ali Kiba aliondoka bila kupafomu. Marioo alipewa mic isiyo na betri. Kuna watu walikuwa na lengo la kuhakikisha wengine hawafanyi vyema,” alisema Mwijaku.

Mwijaku pia alizungumzia kuhusu Ali Kiba, akisema kwamba yeye ni msanii bora katika kuimba live kuliko hata Diamond Platnumz. Alisema kauli hii inatokana na Master Jay, ambaye alisema kuwa Ali Kiba ni mbana pua hawezi kuimba live.

Kwa upande mwingine, Mwijaku alieleza kuwa Ali Kiba aliondoka kwenye Tamasha hilo kwa sababu aliona kuwa hakuwa akiheshimika vya kutosha, jambo ambalo lilichangia zaidi kumtetea Marioo, akisema kwamba matatizo ya kiteknolojia ndio yaliyoathiri sana onyesho la msanii huyo.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *