Mombasa, June 18- Enock Bella, msanii aliyekuwa kwenye kundi la Yamoto Band ambaye kwa sasa yupo Pwani mwa Kenya kwa ziara yake, ameweza kufunguka mengi kuhusu safari yake ya muziki.Debase ambaye alikuwa kwenye kundi na wasanii kama vile Mbosso,Aslay na Beka flavour na kuvuma kote Afrika kupitia ngoma zao,amesema hakuna uwezekano wa kudi hilo kurudi pamoja kama zamani.

Kupitia kipindi chetu cha The Rush Hour,Enock ameweza kumtaja mtayarishaji muziki maarufu Afrika Mashariki,Shirko kuwa mmoja kati ya waanzilishi wa Yamoto band.Kulingana na Bella,shirko ndio mtu wa kwanza kumtambua na kumpatia nafasi ya kuingia studio na kufanya ngoma yao ya kwanza inayoitwa ‘Ya Moto’ ambayo ilikuwa na muundo wa kipekee.

Debase amempa maua yake mtayarishaji muziki na msanii huyo na kuongezea kwamba wasanii wa humu nchini wanafaa kufanya kazi na Shirko kwani yuko na kila kitu ambacho msanii anahitaji.
‘Wasanii na wanasanaa wote hapa Kenya wanastahili kufanya kazi na Shirko kwa sababu yuko na uwezo mkubwa sana,kule tanzania yuko an heshima kubwa sana.Yeye ndio ameizaa Yamoto na kunifanya mimi niwe hapa kama Enock bella,’amesema Enock bella.

Mbali na gumzo kuhusu Shirko,Debase amezungumza pia kuhusu kusainiwa na lebo.Kulingana naye,endapo kutatokea lebo ambayo iko na baadhi ya vitu ambavyo anahitaji basi hatokuwa na budi kusainiwa ila kwa sasa,ameweka wazi kwamba hawezi kubali kuwa kwenye lebo inayomilikiwa na msanii mwenzake.


‘Management ama lebo ikiniafuata nitaangalia mkataba uko na nini na nini lakini siwezi kuingia kwenye lebo inayomilikiwa na msanii kwasababu akiwa msanii hatakubali umshinde kikazi.Akiwa mtu mwengine kwenye sanaa tu sawa lakini msanii mwenzangu,haopana,’ameongezea.

Enock ameelezea kilichomkuta miaka saba iliyopita baada ya kulaghaiwa kusainiwa kwenye lebo inayomilikiwa na Mburundi.Anasema aliitwa na lebo hiyo ambayo iko na ofisi zake nchini Tanzania na kupewa hadi kartasi za mkataba na kuweka sahihi yake akiwa na wakili wake ila baada ya hapo hakuna kilichofuata.Anasema baada ya miezi kadhaa akagundua kwamba walikuwa wezi tu na hakuna msaada wowte waliompa jambo ambalo lilimfanya kukaa kimya bila kuachilia ngoma.

Vile vile amezungumza kuhusu ukaribu wake na wasanii wenzake waliokuwa pamoja kwenye kundi la Yamoto an kusema bado wapo vizuri,wanaongea na kusaidiana panaposatahili.Kulingana nae,Mbosso ndio msanii ambaye wako kwa ukaribu zaidi kwasababu baada ya Yamoto kuvunjika,hao ndio waliopata taabu kupata lebo ya kuwasimamia baada ya Aslay kuchukuliwa,Beka flavour nae kuchukuliwa.

Debase amefutilia mbali tetesi za kwamba anaishi nchini Kenya sasa hivi na kusema kwamba amekuja tu kwa matembezi na kupata upepo mzuri pamoja na familia yake wala hajahamia huku.Kwa sasa msanii huyo ametoa ngoma kibao tu ikwemo Sauda,I swear,ngoja kidogo na nyenginezo.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *