Mombasa, June 19- Antony Tandiko almaarufu Ziky Mtanah,msanii wa kizazi kipya na mzawa wa Pwani mwa Kenya ameendelea kuwa gumzo hata baada ya kuwa kimya kwa muda.Ziky ambaye alijulikana kupitia ngoma yake ya ‘mama wanangu’ amekuwa miongoni mwa wasanii ambao wako na mashabiki wanaowakubali muda wote.
Ziky Mtanah ambaye pia ni mmiliki wa Tanah Empire ambayo ilikuwa na wasanii kama vile Roki amekuwa akifanya kazi na kuendesha sanaa kwa kujitegemea kwa muda mrefu.Tanah Boy amefanya kazi hivi karibuni na wasanii wakubwa kama vile Susumila ambayo ilimuongeza umaarufu zaidi kupitia ngoma hiyo inayoitwa ‘Can We.’
Hata hivyo,mwezi uliopita kupitia mahaojiano kwenye The Rush Hour, Ziky alisema wazi kwamba ameshindwa kuachilia kazi mpya baada ya mitandao yake hasa ya kijamii kudukuliwa.Ziky alisema kwamba bado juhudi za kuipata mitandao yake zinaendelea huku akiwa hana matumaini.
Ikumbukwe kwamba, Ziky alifaa kuachilia kolabo yake na Echo254 ambayo alikuwa tayari ameigusia na kuwaacha mashabiki na kiu ya kutamani kuiskia.Ziky ameamsha mitandao na kuzua gumzo mapema leo baada ya kuidondosha rasmi ngoma hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu japo kuna utofauti wa mitandao ambayo imeibeba ngoma hiyo.
Kupitia mazungumzo ya moja kwa moja na Yugebwize kwa njia ya simu, Ziky amefunguka kwamba ameweza kusainiwa rasmi na Limelight Studios iliyoko Jijini Nairobi.Kulingana na Ziky Mtanah,yuko na matumaini makubwa kuhusu kutimiza ndoto zake zaidi kwenye sanaa.
Msanii huyo ameisifia lebo hiyo na kubana jina la mmiliki ila amesisitiza tu kwamba inamilikiwa na kigogo, tajiri na mtu mwenye uwezo wa kumfikisha Ziky kimataifa kupitia muziki wake.
Msanii huyo vile amesema kwamba baada ya kuingia kwenye maktaba na lebo hiyo, wakaamua kuachilia ngoma yake ya kwanza ambayo ilikuwa imetayarishwa na Producer Wakidigo huku akiwa ameshirikisha Echo254 ngoma yenyewe inatwa ‘marry me’ ambayo ndio hii hapa unaweza kusikiliza https://youtu.be/XmiTAa9A9t0?si=m7BDfoLRq744rCbK
Limelight Studios ni miongoni mwa kampuni zinazofanya video za muziki, kurekodi na kutengeneza ngoma na pia kuwasaidia wasanii kusikika mbali zaidi. Limelight ilianza miaka kadhaa iliyopita japo kupitia mtandao wao wa Youtube wameanza rasmi na wimbo mpya wa Ziky Mtanah.