Mombasa, Agosti 1 – Msanii Kelechi Africana anaendelea kuzua gumzo kwenye mitandao kutokana na machapisho yake ya hivi Karibuni zaidi.Mashabiki na wadau mbali mbali wa sanaa wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusuiana na kauli ya Mr Bwii kwenye mitandao.
Kelechi ambaye alikuwa ameahidi kudondosha albamu yake ya pili ndani ya mwaka mmoja bado haijaidondosha.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Sound chief ameeleza sababu ambazo zimefanya hajaachilia album hiyo hadi sasa.
Ameandika hivi kwenye mtandao wake wa facebook,’Dah kutoka nitangaze nawaachia album,koo langu halifanyi kabisa, sauti haitaki, homa sio homa…naona kama nimebadilishiwa sauti nikapewa ya Kidis.’
Saa chache badae,Kelechi ameweza kuandika kwamba pia anahitaji maneja wa kike ambaye yuko na pesa. Kauli hii ameadnika siku moja baada ya kuelezea kwamba hajakuwa na mtu ambaye ameweza kumsimamia inavyostahili.Kulingana na Kelechi,mambo mengi kuhusuiana na muziki wake,amekuwa akiyafanya mwenyewe bila maneja.
Sound Chief ametangaza kupitia mtandao wake kwamba anafuta maneja wa kike mwenye hela kwani wanaume wamekuwa wenye maneno mengi.Ameandika hivi,’Natafuta manager wa kike,awe na hela.Managers wengi wakiume hawana hela story tu ndio nyingi.’
Kauli yake imeweza kuzua gumzo huku wengine wakidhani Kelechi yuko na malengo tofauti huku wengine wakimuombea apate usimamizi mzuri anaouhitaji ili kutimiza malengo yake kwenye muziki.
Suala na maneja ni miongoni mwa mambo ambayo yanazungumziwa nchini baada ya Mumbi Maina, aliyekuwa maneja wa Otile Brown kutangaza rasmi kwamba amejiondoa.Kila mtu sasa anaendelea kusubiri kama Otile atamtangaza nani tena kama msimamizi wake.