Mombasa, Kenya, Oktoba 16- Mwanahabari, mwanablogu na pia muundaji wa maudhui kwenye mtandao wa Youtube ukanda wa Pwani Tizo Wa Leo, ameweza kufunguka kuhusu ugumu wa kazi na changamoto wanazopitia kama wanablogu hasa hapa Mombasa.

Kupitia mahojaino kwa njia ya simu kwenye kipndi cha The Rush Hour siku ya Jumanne 15 Oktoba 2024, Tizo ameweza kuijibu kauli ya Blogu mwenza Captain Nyota ambaye aliitoka Mombasa kwa sasa.
Kulingana na Nyota, alizua gumzo kwamba sanaa ya pwani ni ngumu kwa ukosefu wa ushirikiano baina ya washikadau. Aliandika kwamba wasanii wengi mambao anawafanyia mahojiano hawasambazi hizo video za mahojiano yaojambo linaloifelisha sana ana kuwatoa moyo wa kuendelea wanablogu.

Tizo kwa upande wake, ameunga mkono kauli hiyo na kusema kwamba wasanii hawasaidiki.
“Bro wasanii hawasaidiki, tunawapatia support lakini hawatupatii support hata kwa kushare kazi zetu ambazo huwa ni interviews zao,” Tizo amesema.

Tizo pia vile vile ameongezea kwamba ugumu huo umechangaia kukosa biashara kama wanavyozipata wenzao jijini Nairobi. Ameweza kuwaomba washikadau wa sanaa kuja Pamoja na kuongeza ushirikiano pia kwa wanablogu kwani wana mchango mkubwa kwa jamii na kutuhabarisha habari mbali mbali za kila upande.

Sio huyo tu, tulibahatika kuzungumza na Van mmiliki wa Van Tv online ambaye pia anafanya kazi nzuri ambaye pia malalamishi yake yalikuwa hapo hapo kwa kutusaidiwa licha ya wao kuwa msaada mkubwa.


“Ni kweli bro wasanii wanavimba ,tunawasaidia lakini hawatuspport kabisa,” amesema van.

Haya yanajiri huku wanablogu wengi wakihisi jijini Nairobi kuna upenyo wa mafanikio kuliko pwani.K wa muda sasa, Captain Nyota hajakuwa akiweka video za wasanii kiama awali.Machampali pia hajakuwa akijisumbua sana na masuala ya wasanii licha ya kuwa na uwezo mkubwa.

Kwa upande mwengine wanablogu wamekuwa wakiwekewa lawama ya kuandika habari ambazo hazijathibitishwa. Kauli ya hivi punde zaidi imetoka kwa mwanariadha Ferdinand Omanyala ambaye ametoa wito kwa wanablogu kuandika habari ambazo ni za kweli. Omanyala amesema baadhi ya blogu huandika mambo ya uongo na kuwaharibia watu majina.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *