Mombasa, Kenya, Januari 21- Msanii wa kizazi kipya, Chipukizi kutoka ukanda wa Pwani, Qaccim Dikei afunguka kuhusu safari yake ya muziki. Dikei ambaye amevuma kupitia ngoma yake ya Usikwa wima,aliazna kupata umaarufu zaidi mwaka jana baada ya ngoma hiyo uingia kila kona.
Usikwa Wima aliifanya na Timatsi kisha badae wakairudia upya wakiwa na K.O kenya ambapo iliongoza kasi na utamu hivyo basi kuskiliza na kupendwa na watu wengi zaidi. Kulingsana na Dikei,remix hiyo ilichangiwa pakubwa na msanii Happy C ambaye alimuunganisha Qaccim na K.O na kuifanya kazi hiyo.
“Remix ya Usikwa wima hata ni producer wangu ndio aliniambia Happy C ametoa pendekezo la kuifanyia remix na K.O ambapo sikuwa naweza kubisha kwa sababu producer alikuwa ndio kusema,basi akaja studio tukapiga kazi na ikatoka,” aelezea Qaccim.
Msanii huyo mzawa wa Kaunti ya Kwale, ameachilia kibao chengine ‘Muvyere’ ambacho pia kinaendelea kufanya vyema. Amesema ameamua kuipatia thamani lugha ya kiduruma kama zinavyoheshimishwa lugha tofauti tofauti kote duniani. Qaccim atakuwa ameingia kwenye kundi la wasanii kama vile Mr Bado, Pero, Nadi, Amoxco, Reagan Dandy na wengineo kwa kutumia lugha za kimijikenda kwenye kupitisha ujumbe kupitia muziki.
Akizungumza kwenye The Rush Hour siku ya Ijumaa,tarehe 18 Januari 2025,Qaccim amefunguka kwamba kwenye amefika saa hii,hawezi kubali kufanya show ambayo malipo ni shilingi elfu kumi.
“Siwezifanya show yenye nalipwa Elfu Kumi,hiyo nikujidharau kwasababu hata kufanya ngoma siku hizi haitoshi na pia niko na manager wangu anafaa pia apate kitu hapo. Sikufanya shows mwaka jana December lakini hata zikianza kuja ile ya chini kabisa naweza chukua ni 50k, japo kuna kuelewana,” amesema Qaccim Dikei.
Ikumbukwe kwamba kufikia sasa,msanii huyo yuko na ngoma mbili amabzo zimetesa anga huku akitoa ahadi kwamba mwaka huu utakuwa wake kwani kazi zipo nyingi na kubwa.
Qaccim amewashi kufanya kazi na Trilly Trillinaire lakini pia mbali na usanii, yeye ni mfanyibiashara na pia muigizaji.
Amesema kwa sasa,anaekeza nguvu nyingi kwenye usanii hadi mambo yanyooke kisha ataendelea pia na uigizaji.