Mombasa, Februari 5- Nesphory Simbiga, maarufu kama Kidis The Jembe, msanii maarufu kutoka Tanzania, anazidi kuwa gumzo kila kona. Kidis, ambaye pia anajulikana kwa majina ya Ngenje Kitaa na Jembe, ameibua midahalo mapema leo kupitia post yake kwenye mtandao wa Facebook.

Kidis The Jembe aliandika hivi: “Tizo Wa Leo, watu waache kutumia cheap vixens wanakaa shangazi zao yoh, sio saa siyta ni bulungutu.” Maandishi haya yametokea kutawala majadiliano, kwani baadhi ya mashabiki hawajaelewa ikiwa Kidis alikuwa anazungumzia msanii fulani ambaye alifanya video na vixens wa bei rahisi.

Baadhi ya maoni ya mashabiki wake kwenye mtandao wa Facebook ni kama ifuatavyo:

Sandes: “Kidis, umesahau pia wewe ulikuwa watumia cheap vixens, sasa Mungu kaiongeza imani yako, watumia expensive vixens, Mungu Mkuu.”

Evans Jeff: “Ni sawa na kujipa laana.”

Bemmy: “List ikam faster faster kabla sijakasirika.”

Kidis The Jembe ni msanii ambaye alijizolea umaarufu kupitia ngoma kama “Bonge La Toto”, aliyoifanya akiwa na Shabiggy, ambapo video ilijumuisha wasichana warembo waliokuwa wakifanya kazi nzuri. Hata hivyo, mwaka huu kumekuwa na upungufu wa video nyingi kutoka kwa wasanii, kwani wengi wameachilia audio kwanza.

Zaidi ya hilo, Kidis amekuwa akizungumzia matukio mbalimbali, hasa mwaka jana mwezi Desemba, kuhusiana na masuala ya MCSK na maandamano ya kushinikiza kuondolewa kwa viongozi wanaofinya wasanii.

Kidis The Jembe alijulikana zaidi kwa kuingia kwenye Kwale Stadium kwa gari aina ya Range Rover wakati wa Rashid Abdallah Supercup, jambo lililozua gumzo kwa takriban mwezi mzima wa Desemba. Wengine walimuita msanii wa Range Rover, huku wengine wakikanusha kwamba alikuwa na uwezo wa kumiliki gari hilo.

Hata hivyo, kwenye tamasha hilo, wasanii kama Jay Melody, Nandy kutoka Tanzania, na Kelechi Afrikana walikuwepo, na wote walikuwa na magari aina ya Range Rover, ingawa hawakuonekana kwenye tukio hilo.

Baada ya hapo, Kidis alikubali msamaha kutoka kwa msanii mwenzake Kelechi Afrikana, ambaye alikiri kosa kupitia mtandao wa Facebook na kuomba msamaha kwa wasanii wenzake na wadau wa muziki kwa lolote alilowakosea. Kidis alikuwa miongoni mwa wasanii waliokubali msamaha na kuendelea kusukuma mbele muziki wa Kiswahili.

Kwa sasa, Kidis Ngenje Kitaa ametangaza kolabo na wasanii wanaochipukia kwenye muziki, huku akiongeza matumaini kwa kolabo kubwa na Plannet Kenya na Tommy Flavour, ambayo inasubiriwa kwa hamu.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *