Mombasa, Februari 18- Msanii tajika humu nchini mzawa wa Kaunti ya Kwale,Kelechi Africana anazidi kupiga hatua kimuziki kwa kuachilia kazi mara kwa mara.Kelechi ambaye ni miongoni mwa wasanii waliobobea kwenye uimbaji wake na utunzi wa ngoma amedokezea kuachilia album yake kabla mwezi huu wa Februari kuisha.
‘Made in 002,Diani’ ndio jina la album hiyo ambayo itakuwa inadondoka hivi karibuni.Kulingana na Kelechi Africana,album hiyo itakuwa kubwa kama album zake za awali.
Kupitia mahojiano ya kipeke kwa njia ya simu na Dullah Waghettoh kwenye The Rush Hour,Jumatatu 17 Februari,Kelechi amefunguka kwamba ‘Made In Diani’ imebeba ngoma 22 na bado anaona akiongheza mbili kama bonus tracks.
‘Album iko na nyimbo 22 lakini naona nikiongeza zengine mbili ziwe 24 kwa sababu niko na ngoma nyingi.Kwanza naweza amua siku moja niachilie album ya ngoma 50 manake niko na ngoma nyingi sana.Hata baadhi ya ngoma kwenye album ni za mwaka jana,’amesema Kelechi.
Kwenye album hiyo vile vile ametaja kwamba imejaa kolabo na remix ya ngoma zake kwenye album ya mwaka jana ya ‘I,am the president’ a kusema kwamba amerudia baadhi ya ngoma zilizofanya vyema kwenye album iliyopita.
Ikumbukwe kwamba hii itakuwa album yake ya nne ,baada ya kutoa ‘The Soundchief Experience’ yenye ilikuwa na ngoma 22,’Keep it Fleek’ yeye ngoma nane,kisha akaja na ‘I,am The President’ yenye ilibeba ngoma 25 na hivi karibuni itakuwa na nyimbo 22.
Huenda ikawa ni rahisi kwa msanii kama Kelechi kuachilia album kila mwaka kwa kuwa yeye pia ni mtayarishaji muziki na yuko na studio yake ya Fleek Made It ambayo huenda ikawa inachangia yeye kuwa na kazi nyingi.Lechi amekuwa miongoni mwa wasanii walioweka rekodi ya views nyingi kwenye mtandao wa youtube kuwahio kutokea Ukanda huu Pwani kupitia ngoma yake ya Ring ambayo ikon a watazamaji zaidi ya milioni 14.
Kuhusu ushirikiano na wasanii wenzake,msanii huyo ametaja kwamba baada ya Album,atakuwa anakuja na Ep ambayo huenda ikawahusisha wasanii ambao hawakuwa kwenye maelewano ila wakaombana msamaha na kuyasahau yaliyopita.Hii inaamnisha kwamba siku zijazo,tutarajie kolabo ya Kelechi na wasanii kama vile Susumiloa,Kidis na wengineo.