Mombasa, March 19- Shabiggy anazidi kuzua gumzo kwenye mitandao kwa mara nyingine, kupitia posts zake za mara kwa mara ambapo anawaponda wasanii wenzake na washikadau wa muziki wa ukanda wa Pwani.
Hii ni baada ya kuandika maoni ambayo yalizua mjadala mkubwa kuhusu hali ya muziki na ufanisi wa baadhi ya wasanii na bloggers wa eneo hilo.
Shabiggy, ambaye anafanya vizuri kupitia kolabo yake na Kidis kwenye ngoma maarufu ya Bonge la Toto, ameamua kufunguka na kuzungumza waziwazi kuhusu mashabiki na wasanii anaowakubali.
Katika post yake ya hivi karibuni, Shabiggy aliwataja baadhi ya wasanii wa hip hop anaowakubali, huku akiwakosoa vikali wenzake akiwemo Kaa la Moto, ambaye alieleza ni “fake mcees.”
Kwa kupitia video kwenye mtandao wake wa TikTok, Shabiggy alisisitiza kwamba ataendelea kusema ukweli bila kuogopa, hata kama atachukiwa kwa kufanya hivyo. Alisema wengine wanadai kwamba ana kiburi kwa sababu ya kuzungumza ukweli. Alifunguka zaidi kwa kusema kuwa hata bloggers kutoka Pwani wamekuwa wakikosa ukweli kwenye uandishi wao.
Katika post yake, Shabiggy alielezea jinsi mashabiki wengi wa muziki wa Pwani wanavyokuwa wakikosoa wasanii na kuchanganya kiki na ukweli. Aliandika:
“Mashabiki wa Coast kibao ni wasanii under ground, matusi kibao, na hawana muda wa kudadavuwa hoja. Jueni kutofautisha kiki na ukweli. Comments kibao ni za watoto wa elfu mbili na hawajui kitu. Ropo nyingi, wacheni kucrown wacheza gololi wakati mamcs wa kweli wapo.”
Shabiggy aliendelea kuelezea wasanii kadhaa anaowakubali na kusema kwamba wao ndio wanaweza kubeba mzigo wa kweli wa muziki wa hip hop. Aliwataja wasanii kama Kimbo, Tricks, Ohmzlow, Manjewyne, GiantPandikizi, Kiwanja, Jituzee, Kichashado, na Bozenjemedari. Alisema:
“Wengine mnawaita malegend sababu wako center na michingo mashendrrrreea mashendrrrea.”
Kuhusu waandishi wa habari na bloggers wa ukanda wa Pwani, Shabiggy alifunguka kuhusu hali ya uandishi wa habari. Aliandika:
“Mablogger walio baki coast ni wawili, mmoja anapost story za home, mwingine anadai anafukuzia international na ndio ashapitwa. Chanuka usikale ndiya biro, charity begins at home.”
Shabiggy hakuwataja bloggers hawa kwa majina, lakini inasemekana anazungumzia waandishi maarufu kutoka Pwani kama Tizo, Captain Nyota, na Shampuz kutoka Kaunti ya Kilifi. Hii imeibua maswali kuhusu ni nani hasa anaowalenga na namna wanavyoshughulikia maswala ya muziki na habari katika ukanda huo.
Shabiggy aliwataka wasanii wa Pwani kuacha ubinafsi na kujenga umoja kwa ajili ya maendeleo ya muziki wa ukanda huo. Aliandika:
“Shida ni ubinafsi na kujuwana. Tuache tabia ya kubaguwana na kuogopana, tutafika mbali. Hirizi zenu zitumieni wakati wa show mjaze viwanja vya mpira. Mnakokotera hirizi, wasanii wasipendane, mnakokotera hirizi vibaya. Ndio maana game haisongi. Chuki za nyuma ya pazia ni mbaya. Tusiogopane, tumuogope ALLAH pekeake.”

Nitaendelea Kuongea Ukweli, Siogopi Kuchukiwa – Shabiggy Asema
Shares: