Mombasa, Novemba 4- Kampuni ya utengenezaji Pombe ya East African Breweries PLC (EABL) imezindua rasmi kampeni maalum,iitwayo “It’s A Wrap” katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo jijini Nairobi.

Kampeni hiyo ya kila mwaka inaashiria mwanzo wa msimu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya za mwaka huu.


Hafla hiyo iliwaleta pamoja wafanyakazi wa EABL, washirika wa kibiashara, vyombo vya habari na washirika wengine ambapo kampeni hiyo ya mwisho wa mwaka inalenga kuenzi mafanikio na hatua muhimu ilizopiga mwaka huu na kupongeza ari ya maendeleo na umoja ambao ni nguzo kuu ya ukuaji wake.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,mkurugenzi mkuu wa masoko na ubunifu wa EABL Mark Mugisha,amesema kampeni hiyo almaarufu “It’s A Wrap inasisitiza umuhimu wa ushirikiano baina yao na washirika wengine kufanikisha ukuaji,utendakazi bora na mafanikio ya kampuni hiyo.


Wakati huo huo Kampeni hiyo imezileta pamoja bidhaa zilizoko chini ya EABL ambazo ni:Johnnie Walker Black, Blue and Gold, Don Julio, The Singleton, Gordon’s London Dry Gin, Baileys na Smirnoff.
EABL imeahidi wateja wake kuboresha zaidi huduma zake, kuona kwamba inafikia malengo yake.


Kwa upande wao washirika wa hafla hiyo,walielezea mafanikio ya mwaka huu,wakipongeza EABL kwa kujitolea na kuimarisha utendakazi wake hasa katika masuala ya ubunifu,uvumbuzi na uwajibikaji.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *