Mombasa, March 12- Msanii wa nyimbo za injili Ramadhan Karisa,maarufu kama kaytozy amefunguka kuhusu changamoto ambazo wasanii hupitia kwenye maisha yao ya sanaa.

Kupitia video kwenye mtandao wake wa Facebook,ameelezea kwamba wasanii wanateseka licha ya kuonekana wamevaa nguo za ghali na kuishi maisha mazuri.Kulingana na kaytozy,wasanii huvaa hivyo kwasababu muziki unahitaji muonekano mzuri ila haimaanishi kwamba wanaishi vizuri.

‘Mkiona msanii amevaa vizuri haimanishi muache kumsupport,kuvaa vizuri huwa si kupenda kwetu, tunavaa kwasababu kazi yeu ndioi inafanya tutafute muonekano mzuri na hiyo haimaanishi kwamba tuko sawa,’amesema kaytozy.

Hii inaashiria kwamba maisha ya familia za wasanii zinaishi kwa shida licha ya msanii kujiweka vizuri mjini kama hatapata uungwaji mkono wa kutosha.Hata hivyo,ameweza kuwaomba mashabiki kuendelea kuwashika mkono wasanii kwa kuskiliza na kusambaza ngoma zao ili wapate kipato cha kuishi maisha ya kweli na halisi.

Kaytozy ametoa mfano wa Kaluma Boy,kijana aliyesaidiwa na wakenya kutokana na changamoto anazopitia pamoja na familia yake na kusema kwamba si lazima msanii afikie hatua hiyo ndio apewe msaada.

‘Msingojee mpaka msanii apige picha za mazingira ya kwao anakotoka ama ya jinsi wazazi wake wanavyoteseka ndio mumpatie support,hata sisi ambao mnaona kama tuko vizuri tunahitaji mtu support kwasababu hatuko vizuri,’ameongezea Kaytozy.
Vile msanii huyo ambaye ndio wa kwanza kutoka Pwani kufanya kolabo na Guardian Angel,amefunguka changamoto alizopata wakati akikutanishwa na msanii huyo mkubwa.

‘Tukiwa kwa gari tukielekea kukutana na Guardian Angel,mwenye alikuwa ameniunganisha,alikuwa amelazimisha nivae matambara ili Guardian Angel akiniona eti anionee huruma,mimi sikuvaa matambara kwasababu tayari nilikuwa napenda kuonekana vizuri,’amesema msanii huyo.

Kiukweli,wapo wasanii ambao wanavaa vbizuri ila wanahitaji kuskilizwa na kusaidiwa ili kutimiza ndoto zao kimuziki kw3ani wengine huishia kukata tamaa na kuacha kabisa kufanya muziki.

Kaytozy vile vile anatarajiwa kuachilia ngoma yake mpya kwa jina ‘uzima’ ambayo imetayarishwa na Emmy dee mmoja ya watayarishaji muziki mashuhuri humu nchini.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *