Mombasa, Kenya, December 16- Msanii wa Gengetone kutoka ukanda wa Pwani,Ashley Queen amefunguka kuhusu gharama za wimbo wake mpya.Tepe Tepe ni wimbo wa hivi punde zaidi ambao unaendelea kufanya vyema kupitia mitandao mbali mbali.
Akizungumza kwenye kipindi cha The Rush Hour siku ya Ijumaa tarewhe 13 Disemba 2024,Ashley amesema Tepe Tepe ni miongoni mwa nyimbo zake zilizotumia pesa ndefu zaidi mwaka huu.
‘Video yangu ya Tepetepe tumeshoot locations zaidi ya tatu,vixens naos io wa mchezo mchezo,gharama zote bila kuweka za mafuta,nilitumia kama 959k,’amesema Ashley.
Ashley ambaye amekuwa akionekana kama msanii wa kike mwenye hela Pwani nzimamameweza kukanusha kwamba yeye ni mpambanaji tu ambaye anajaribu kujituma kupitia biashara na kazi mbali mbali.
Ashley ambaye amesema yeye hufanya kazi ya mjengo ambayo pia ilikuwa gumzo siku chache zilizopita,amesema haikuwa kiki ila kazi kamili.
‘Mimi najituma,nafanya mjengo na hustles zengine hata saa hii nafikiria kufungua kibanda cha mboga.Wanaosema mimi ndio Tajiri kwa wasanii kike ukanda wa Pweani wanasema ila mimi sijui,’amejitetea Ashley.
Queen amenyoosdha maelezo kuhusu mahusiano na msanii mwenza K.O na kusema kwamba walikuwa wanaskuma ngoma zao tu.Amefunguka kwamba hawakuwa kwenye mahusiano yoyote na kueleza kwamba hiyo ilikuwa kiki tu.Ashley ameelezea kwamba muziki umekuwa na mambo mengi na wakati m wengine unahitaji matukio kidogo ili uendelee kuzungumziwa.
Msanii huyo amewezxa kuwataja Watanzania kama watu ambao sanaa yao iko juu kutokana na matukio ambayo hufanya ili kuskuma muziki wao.Ameongezea kwamba ipo haja ya mashabiki wa nyumbani kukumbatia matukio ya wasanii wao ili kufikisha muziki mbali.
Vile vile msanii huyo ametaja urafiki wake na Ella Shikanda kwamba wako na ushkaji na wako na kazi ambazo watakuwa wanaziachilia kuanzia mwaka ujao.Ashley anasema ameamua kubadilika na mashabiki watarajie ngoma za injili kuanzia mwaka ujao.