Mombasa, Februari 14- Steve Kipande, mwanamuziki maarufu na mwenye uzoefu kutoka ukanda wa pwani ni miongoni mwa washikadau wenye busara za kunyoosha maelezo na kuwa wazi hasa kuzungumzia mambo yanayoendelea kwenye sanaa.

Steve ambaye jina lake la usanii ni Daddy Q ni miongoni mwa wasanii walioupa muziki wa pwani heshima miaka ya nyuma, sasa hivi Steve anajishuhulisha na masuala mengine kama vile kutengeneza filamu kama video director, kufanya video na kupiga picha, yupo na duka lake la nguo-Grip Wear Clothing na mambo mengi tu .

Kupitia mahojiano kwa nnia ya simu kwenye Celebrity check Up ndani ya The Rush Hour inayofanywa na yuge na Dullah Waghetto,Kipande amefunguka kuhusu sanaa ya pwani ya wakati wao na sasa kwamba upo utofauti mkubwa.Akitaja kwamba anaungana na wanahabari kusherehekea siku ya Redio Duniani kwani imekuwa yenye mchango mkubwa sana kwa wasanii kwani wakati wao hawakuwa na mitandao kama sasa.

Kulingana na Steve,Redio itabaki kuwa redio kwa miaka zaidi ijayo tofauti na inavyosemekana kwamba rdio zimeisha nguvu. Daddy Q amesema redio haziweshi shindwa nguvu na mitandao kwasababu kwa sasa redio pia zipo mitandaoni.

Ameisifia idhaa hiyo ya redio ni kusema imechukua nafasi kubwa sana kwa sanaa yetu akitaja kwamba kitambo ilikuwa rahisi wasanii kujulikana kupitia redio kwasababu walikuwa kidogo tofauti na sasa.

Kupitia mahojiano hayo hayo,Daddy Q amezungumza kuhusu matukio yanayofanywa kutoka mkoani pwani kwamba yanakosa ubunifu wa kutosha.Steve hajawakashifu wasanii,amesema tu kwamba wanahitaji kuwa na timu ya watu wanaowasaidia kwenye kufikiria na kuandaa matukio ambayo yatashtua watu wengi kutoka maeneo tofauti ya Kenya sio Pwani pekeake.

Daddy Q hakutaka kutaja msanii yeyote ila ametoa mfano wa msanii Susumila kwamba hajawahi kufanya ‘kiki’ na amekuwa akipata matamasha sehemu mbali mbali humu nchini.Amemtaja kama mfano bora wa kuigwa huku akisema wanaohitaji kufanya matukio wakae na waandike matukio ambayo hayakasirishi shabiki.Kulingana nay eye kuna baadhi ya matukio ambayo akiyaona anakasirika na jinsi yanavyofanywa tu.

Kulingana na Kipande,matukio ni kucheza na hisia za mtu kwa hivyo inafaa mtu afikirie jinsi ya kucheza na akili na hisia za watu bila kuwaudhi.Amesema kwamba wasani wamefanya matukio ya kweli yanaonekane ya uongo na ya uongo Yazidi kuonekana uongo.Ameweza kutoa ushauri kwa wasanii kuzingatia muda ambao watafanya matukio ili madhumuni yasiwe ni kuachilia ngoma tu.

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *