Mombasa, Agosti 26- Msanii aliyekuwa kwenye kundi la Susumila akiwa na Susumila wa sasa,Nasoro maarufu kama Escobar Babake,amezua gumzo kwenye mitandao baada ya video yake kusambaa akifanyiwa mahojiano ya kipekee na mwanahabari wetu Yugebwize kupitia mitandao yetu ya Mo radio.

Escobar amejulikana kupitia ngoma zake ambazo asilimia kubwa huwa hadithi zenye mafunzo kibao.Baadhi ya ngoma za escobar zilizofanya vyema ni pamoja na Vurumisha,Kaka saidi,kaa Chonjo,Amina na nyenginezo.Mwamba amepata umaarufu kupitia matamasha mbali mbali ukanda wa pwani tangu miaka ya nyuma.

Ganje ni mmoja ya wasanii ambao wanatoka kwenye familia ambazo hazikuwa na uwezo mkubwa wa mali ila amejaribu kuibadilisha taaswira hiyo kupitia muziki.Babake ambaye alisoma katika shule ya upili ya Agha Khan na kujizolea alama ya B(plain) japo changamoto ya pesa ilimkosesha nafasi ya kujiunga na chuo kikuu.Kulingana na msanii huyo,ndoto yake ilikuwa kusomea uchora ramani wa nyumba yani Architect.
‘Ndoto yangu ilikuwa kuwa architect ila babangu wakati huo hakuwa vizuri kimfuko ndio maana sikuweza kuenda college ama university,’amesema Escobar.
Hata hivyo,mwamba anajivunia kufanya muziki kwani anasema ulimpatia mapato ambayo alianzisha biashara inayomueka mjini hadi sasa.

Escober pia ajibu swali la kizushi kuhusu kumchagua kati ya Susumila,Kidis na Shabiggy ambapo ameulizwa swali rahisi.
‘Endapo unafaa kufuta namba moja kwenye simu yako ili uweke nyengine na unaambiwa ufute kati ya namba ya Susumila na ya Kidis,unafuta gani uache gani?Ameulizwa ganje.
Akajibu,’Siwezi futa labda ninunue line nyengine lakini kama ni lazima,naweza futa number ya Kidis kwa sababu sina mchongo naye kwa sasa..’

Jibu lake limezua gumzo huku watu wakidhani anaamanisha ila kwa kweli lilikuwa swali la utani tu.
Escobar na Shabiggy wanaendelea na tour yao ya kuskuma wimbo wao mpya ‘Watoto wa Mungu’ ambao unaendelea kufanya vyema.
Kufikia sasa,wawili hao wameonyesha ubora wao kwenye kazi zao ambazo wamekuwa wakiachilia hasa kuanzia bora yupi,sugar na sasa watoto wa mungu

Shares:
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *